imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Huyu Mbunge anastahili pongezi.Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala a
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyu Mbunge anastahili pongezi.Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala a
Mbunge wa Viti Maalum, Kunti Majala ameshauri mamlaka zinazosimamia misafara ya viongozi, kuwasiliana ili kupunguza muda wa watu kusimama njiani wakati wakiwasubiri wapite.
Mbunge huyo ameyasema leo Aprili 12,2023 wakati akichangia mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.
Mbunge huyo amesema viongozi wao wanawaheshimu, wanawapenda na wanajua changamoto zao kwa majukumu yao wanayoyafanya lakini watu husema muda ni mali.
“Kusimamisha wananchi zaidi ya saa tatu barabarani, kiongozi hajatoka anatokako, tuna wagonjwa, kuna watu ambao wanatakiwa kwenda kutekeleza majukumu yao mbalimbali.
“Niwaombe viongozi wanaosaidia hususani wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Polisi, biashara ya kusimamisha magari, mabasi na wananchi wengine kwa ajili ya viongozi wetu wanapopita wawe wanawasiliana kwa kadri muda unavyosogea wawaache Watanzania (wapiti),”amesema.
Amesema leo Waziri Mkuu alikuwa anatoka nyumbani kwake kuanzia saa 2.17 magari yalisimamishwa ambapo foleni imefika hadi Nzuguni na kuhoji hilo linapandisha uchumi.
Amehoji kama angeamua kutumia magari kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, wananchi watasimama kwa muda gani.
“Niombe sana hivi vitu vingine tuwe tunaenda na wakati. Kwa safari (viongozi), ndefu watumie ndege waache kutumia magari,”amesema.
Akitoa taarifa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema suala la kusimamia usafiri wa viongozi liko katika mamlaka zinazohusika.
“Nadhani ingekuwa ni bora kwa mbunge kutoa ushauri kwa mamlaka badala ya kuhusisha na utendaji kazi wa viongozi wetu ambao umewekwa kwa utaratibu unaozingatia heshima ya viongozi wetu hapa nchini,”amesema.
Amesema ni utaratibu huo uko dunia nzima na kwamba utaratibu huo umekuwa ukitumika kutoa heshima kwa viongozi.
Hata hivyo, akiendelea kuchangia Kunti amesema wananchi ndio wanaona adha na hivyo wakiamua kuuchukua ushauri huo ni sawa na pia ni sawa.
Chanzo: Mwananchi
Tatizo Teuzi za kupewa, uwezo hana.JENESTER Mhagama huyu mmama sijawahi kabsa kumukubali yaani huwa anamajibu yakukatisha tamaa tu hata kama jambo liko wazi kama hili la misafara ya viongozi imekuwa kero kubwa sana kwa wananchi
Huu mama ni Mzigo. Ninashauri katiba mpya mtu aliteuliwa na Rais jina liende bungeni kupigiwa kura kuepuka kuongozwa na watu wasio na uwezo.Tatizo Teuzi za kupewa, uwezo hana.
mizizi yake itakua imejichimbia chini zaidi ya mingineAngela na Jenista, n moja ya viongoz wasio na sifa serikali ila cha ajabu waliendelea kuaminiwa wizara tofauti. Angela waliamua kumtoa, najiuliza Jenista ana nn, mizizi yake serikalin imeenda mpka wapi,