Bima tayari zinafata mfumo huo tangu zamaniHata bima za gari ziwe hvo hvo
Naona wengi mnampongeza mh Ally Kesi.. ili hali hata yeye alichokiongelea ndicho kinachofanyika.. na cha kushangaza zaid na yeye wazir aakajibu kua atalifanyia kazi (kwa maana halisi na yeye hajui nin alichokua anakijibu..)
Road License ipo miaka mingi sana kweny mafuta.
Hapo zamani license ilijulikana kama Road Toll. Na zilikua zinatozwa kwny vizuizi.. na miaka hiyo watu walipiga sana hela.. ndo katika kurekebisha hlo ndo ikaingizwa kwny mafuta...
Alichokua anazungumzia Mh Kessy bila shaka ni VEHICLE LICENSE...naona na wachangiaji wote mmekimbilia huko huko..
Hii kitu ipo siku nying tu kwenye mafuta..
Nipo tayar kurekebishwa endapo nitakua nimepotosha..
Umeiweka vzur,mkuuUmepotosha sana. Motor Vehicle License ndiyo Road License ambayo hulipiwa TRA kupitia sasa Mobile Pesa au MaxiMalipo au agents wengine waliokubaliwa, na hulipwa kwa mwaka bila kuruka hata sekunde moja na cha kushangaza inachanganywa na fire ambayo sijui hata kama inaleta maana kuwapo pale. Sasa uzi huu ulilenga kujadili ikiwa gari limeegeshwa nyumbani na halijatumia barabara mathalan hata kwa miaka kumi ile kodi inajirudia na kutozwa hata adhabu pasipo kujali matumizi ya barabara. Hili ndilo suala mezani na kuainisha jinsi ulivyopotosha.
Ikiwekwa sasa hili tozo katika mafuta litakuwa kwamba kama gari haitembei basi haitumii barabara na hivyo itakuwa inatoa haki sana na italeta maana au mantiki.
Jadili kuanzia hapo mkuu.
Naomba kuwasilisha
Duuuh...hii nayo imekaa vip...wadau....hizo mashine ambazo hazitumii barabara maybe they are static....lakini wanatumia mafuta..hii kodi ikiingizwa huko si watalipa na hawa ambao hawahusiki?Kutakuwa na vituo vya aina mbili. Vtuo vya mafuta vya wenye vyombo vya moto (gari,pkpk nk), Na vituo vya mafuta kwa ajili ya majenereta na vifaa vingine visivyotembea baraabarani????
NINAUNGA MKONO HOJA 100%. KUNA KIJANA ALIACHIWA CANTER TRUCK MIAKA 5 ILIYOPITA. ILIKUWA YA URITHI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI,WAKATI HUO AKIWA NA MIAKA 14. ILIPAKIWA HADI AMALIZE SEKONDARI. MWAKA JANA KAMALIZA SHULE, KAIFANYIA SERVICE AANZE KUITUMIA,KADAKWA NA JAMAA,WA KODI ANADAIWA ALMOST 4M DENI HUKU HAIJATEMBEA WALA KUFANYA KAZI YOYOTE! SIJAJUA KAMA ATAIUZA ALIPE DENI AU VIPI.
KWA HIYO WAZO HILI LIKIPITA,LITAOKOA WENGI,NA SERIKALI ITAPATA MAPATO ZAIDI.
Katika mambo muhinu yatakayoleta pesa bila shida ni hilo na uhalisia let's say hata wakiweka shilingi hamsini tu watapata income kubwa sana! basi inayotumia 600 lts a day italipa 30000 Kwa siku times 30 Kwa mwezi pekee itakua 900000 Kwa mwaka ni hela ya kutosha! na wakifanya hivyo hata machines zisizo fika barabarani zitachangia pato kubwa LA taifa! imaging machines za migodini per day wanatumia mpaka Lita 10000 plus hivi watasumbuana na daladala kweli! please wabunge amkeni itasaidia all way out
Daah hatimaye ahsantr Mungu..Hii ni moja ya michango bora katika Bunge linaloendelea sasa. Hamna gari inayostahili kulipia road licence kama haipo barabarani, cha ajabu wamiliki wenye magari yasiyotembea kwa ubovu ama ajali yangali yanachajiwa road licence na penalty juu na zaidi ya yote hata kama gari langu ni zima ila siko barabarani kwa muda tajwa ya nini nilipie road licence?
Wenye mamlaka jiongezeni kidogo tu, hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.
Hongera mtoa hoja, hongera wabunge wote mwitikio wenu tumeuona, kazi kwenu serikali!!
=====
Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.
"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.
Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.
Sawa ni ushauri mwingine mzuri lakini kuna suala ongezeko la mapato serikalini endapo kodi itaenda kwenye mafuta hulioni hilo? Ni vyema tukubaliane kuwa kodi ndizo zinazoendesha nchi na kuleta maendeleo. Mwaka Jana 2016 wenzetu Ethiopia wamefungua SGR yao tena ndefu. Kenya nao juzi tu wamezindua ya kwao. Na sisi ndo tunatafuta fedha ili tujenge ya kwetu.Ni ujinga kusema road licence iende kwenye mafuta, petrol na diesel haitumiwi na magari tu. Lakin pesa itakuwa kubwa sana.
Kwani ukipaki gari nani aliesema lazima uilipie Road licence, ukipaki gari nenda TRA sitisha usajili mpka utakapoirudisha na haitakuwa ikihesabu.
Mtu anashindwa kulipa pesa ndogo tu ya road licence ulinunia gari ya nini? Ninyi ndio mnanunia matairi ya elfu 20 expired mitaani ilimradi watu wakuone tu na gari
Huu mchango ni wa kijinga, charges za mafuta zitakuwa juu na zitagusa wasio na magari pia. ROAD LICENCE ibaki kama ni kuomba basi ifutwe kabisa ila sio kwenda kwenye mafuta.
Kama gari lako limepaki ukitaka lisihesabu nenda tra wape plate namba zao waambie nimepaki gari, ukirudi itaanzia ulipoishia
Wakati mwingine wachanigiaji wachache maana yake ni kuwa hoja imekubalika sana na hakuna la kuongeza!hoja ya maana sana hii ila imekosa wachangiaji ingekuwa udaku ingekuwa na page kadhaa
Sawa lakini kama alivyojibu jamaa kuna mitambo amabayo hutumia mafuta pia na haina uhusiano wowote na barabaraSawa ni ushauri mwingine mzuri lakini kuna suala ongezeko la mapato serikalini endapo kodi itaenda kwenye mafuta hulioni hilo? Ni vyema tukubaliane kuwa kodi ndizo zinazoendesha nchi na kuleta maendeleo. Mwaka Jana 2016 wenzetu Ethiopia wamefungua SGR yao tena ndefu. Kenya nao juzi tu wamezindua ya kwao. Na sisi ndo tunatafuta fedha ili tujenge ya kwetu.
Uzuri wa Bima inapoisha muda wake na ukalipaki gari siku ya kwenda kulipia tena Bima unaanzia tarehe hiyo hiyo. Tofauti na hii motorvehicle licence ambayo inaanzia pale ilipoishia mara ya mwisho. Hata kama hiyo gari ilipaki miezi 6Bima tayari zinafata mfumo huo tangu zamani