mycall
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 867
- 523
1.Kuna watu wanalipa kodi ya aridhi kwa mashamba wanayomiliki, wakati wengine wanalima bureWengi siyo wamiliki wa vyombo vya usafiri
2. Kuna watu wanalipa kodi ya ardhi walipojenga wakati wengine hawalipi hasa huko vijijini
3. Kuna watu wanalipa kodi ya majengo wakati wengine hawalipi hasa huko vijijini ambako unakuta kuna nyumba za thamani kuliko hata za mjini
4.Watumishi wote wa umma wanalipa kodi inayokatwa kwenye mishahara yao wakati ktk sekta binafsi wachache sana wanakatwa kodi.
Nadhani hakuna sheria au mfumo wa kukusanya kodi utakaogusa watu wote au kuwa balanced usiumize japo sehemu kidogo ya jamii.
Kama Serikali itakubali ushauri huu wa kukusanya kodi kwenye mafuta, watakuwa wameondoa usumbufu na ukandamizaji kwa kiasi mkubwa.