Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 43,233
- 51,648
Hii ni hoja nzuri sana itapunguza sana kero, hata ya kujaza makaratasi kwenye vioo vya magari.
Bado stika ya nenda kwa usalama ...Sirro kazi kwako
Hii ni hoja nzuri sana itapunguza sana kero, hata ya kujaza makaratasi kwenye vioo vya magari.
Ahh sawa mkuuVery Briefed
Hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.
Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.
"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.
Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.
haitawezekani,,, italeta suala la vituo haramu/ feki vya mafuta.,,Kutakuwa na vituo vya aina mbili. Vtuo vya mafuta vya wenye vyombo vya moto (gari,pkpk nk), Na vituo vya mafuta kwa ajili ya majenereta na vifaa vingine visivyotembea baraabarani????
haitawezekani,,, italeta suala la vituo haramu/ feki vya mafuta.,,
Nmecheka kwa sauti [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Waache huko huko kwenye magari, wengine petrol tunanunua kwa ajili ya kuvuta tupate stimu baada ya kufungia viroba.
Wacha kuongea vitu vya kufikirika wapi wanatumia mafuta ya nchi jirani? Au unaongelea hizo gari mbili mpakani.Road license ni kodi ya kutumia barabara, si kila kinachotumia Fuel basi kinatumia barabara!
Kuna Machine kadhaa zinatumia fuel lakin hazitumii barabara sasa kuziongezea kodi ya barabara ni kuongeza gharama za uzalishaji kitu kitakachosababisha Inflation ( Cost pull).
Wale wanaotumia Mafuta ya magumashi ya kutokea Nchi jirani tutakuwa tumewahalalishi kutumia barabara wasizolipia
😀😀😀😀😀 we jamaa umenichekesha sana aisee..We jamaa vipi ww?hela yote hiyo?unataka tutiane umaskini?waweke shilingi tu kwa liter
Ndugu yangu umetisha kwani hata mwenye mashine yakukata majani atalazimika kulipia ROAD LICENCE!!!Kutakuwa na vituo vya aina mbili. Vtuo vya mafuta vya wenye vyombo vya moto (gari,pkpk nk), Na vituo vya mafuta kwa ajili ya majenereta na vifaa vingine visivyotembea baraabarani????
Ndo mawazo ya wawakilishi wetu, halafu wanahimiza kilimo cha umwagiliaji, lile pampu nalo litalipa road licence.Ndugu yangu umetisha kwani hata mwenye mashine yakukata majani atalazimika kulipia ROAD LICENCE!!!
Mbona umekuwa Mkali katika Jambo la kawaida sana?Wacha kuongea vitu vya kufikirika wapi wanatumia mafuta ya nchi jirani? Au unaongelea hizo gari mbili mpakani.
NINAUNGA MKONO HOJA 100%. KUNA KIJANA ALIACHIWA CANTER TRUCK MIAKA 5 ILIYOPITA. ILIKUWA YA URITHI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI,WAKATI HUO AKIWA NA MIAKA 14. ILIPAKIWA HADI AMALIZE SEKONDARI. MWAKA JANA KAMALIZA SHULE, KAIFANYIA SERVICE AANZE KUITUMIA,KADAKWA NA JAMAA,WA KODI ANADAIWA ALMOST 4M DENI HUKU HAIJATEMBEA WALA KUFANYA KAZI YOYOTE! SIJAJUA KAMA ATAIUZA ALIPE DENI AU VIPI.Hii ni moja ya michango bora katika Bunge linaloendelea sasa. Hamna gari inayostahili kulipia road licence kama haipo barabarani, cha ajabu wamiliki wenye magari yasiyotembea kwa ubovu ama ajali yangali yanachajiwa road licence na penalty juu na zaidi ya yote hata kama gari langu ni zima ila siko barabarani kwa muda tajwa ya nini nilipie road licence?
Wenye mamlaka jiongezeni kidogo tu, hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.
Hongera mtoa hoja, hongera wabunge wote mwitikio wenu tumeuona, kazi kwenu serikali!!
=====
Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.
"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.
Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.
Ili kuondoa mkanganyiko, hiyo kodi inaweza kupewa jina lingine kama issue ni jina "road". Kwani mitambo inayotumia diesel au petrol nje ya magari,hailipi kodi? Kama nh hivyo,dawa ni ku harmonize zile kodi kupitia bei ya nishati ya mafuta.Iliwashika papaya. Hii ni baada ya Gvt & TRA KUWA DIGITAL hakwepeki. Ukuweka kwenye mafuta walio na mitambo isiyotembe barabarani vipi
Mafuta yatapanda
Vipi mkiendelea na utaratibu huo kwani kama Gari haetembe report police na TRA
Wengi siyo wamiliki wa vyombo vya usafirihoja ya maana sana hii ila imekosa wachangiaji ingekuwa udaku ingekuwa na page kadhaa