Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE ALOYCE KWEZI ATOA MILIONI 2 KUJENGA CHOO CHA KISASA SHULE YA MSINGI MWAMANSHIMBA
Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Mhe. Aloyce Kwezi tarehe 04 Oktoba, 2024 akiwa kwenye mahafali iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mwamanshimba, Kata ya Ushokola Wilayani Kaliua.
Mhe. Aloyce Kwezi akiwa katika mahafali hiyo aliwaahidi Wananchi wa Kijiji hicho kuwajengea Choo bora na cha Kisasa kwa ajili ya shule hiyo kwani hela ipo.
Awali, Aprili 2024 Mhe. Aloyce Kwezi aliahidi kuchangia Shilingi Milioni 2 na tayari amewachangia Shilingi Milioni 1 ambayo wameitumia kwaajili ya kufyatua Matofali ya Block.
Pia, Mbunge Aloyce Kwezi amewaahidi kuwaongezea Walimu wa Kike maana Walimu walipo wote ni Wanaume. Mbunge ameahidi kuwaombea ujenzi wa nyumba bora za Walimu.
Mbunge Aloyce Kwezi aliwatunza Wahitimu wote kila mmoja kiasi cha 10,000/= na baadhi ya walimu ikiwemo na zoezi la kuwalisha Keki Wanafunzi, Walimu na Wanakijiji.
Wananchi wa Kijiji cha Mwamanshimba wamefurahi kwa ujio wa Mbunge huyo katika mahafali ya vijana wao pamoja na kupokea ahadi ambazo zikitekelezwa zitachochea maendeleo katika Kijiji hicho,wao pia wapo tayari kwa ajili ya kumuunga mkono.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-10-05 at 10.55.25.jpeg78.3 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-05 at 10.55.25(1).jpeg110 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-05 at 10.55.25(2).jpeg106 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-05 at 10.55.26.jpeg109.4 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-05 at 10.55.26(1).jpeg118.8 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-05 at 10.55.27.jpeg91.5 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-10-05 at 10.55.27(1).jpeg122.9 KB · Views: 4