Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K

Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K

Hili inabidi kulishikilia!wanahamasisha Uzalendo ilhali wao siyo wazalendo🤔🤔
Haya ndio madhara ya kuwaachia wazee wanaojiita vijana kutawala nchi!

Tunataka wabunge na Raisi wawe wa kwanza kulipa Kodi.
 
kwanza, nimenukuu kama ilivyo toka kwa mr malisa GJ.

pili, haya ndo mambo muhim ya kujadili huku uraian ili hata baadhi yetu wanapotuumiza wamejifungia wajue nje tunajua.

tatu, kama kuna uhalali wa madaraja kihivi basi tusipotoshane. kuambizana ukweli ni utamadun unaopotea kwa kas kizaz hiki, tufanye kitu. Kenya wananchi waliwai kufanya kitu kuhusu kuibiana kati ya walipa kodi na watunza kodi.

#NUKUU: UPUMBAVU ni nini? Upumbavu ni huu. Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K kwa siku na posho ya kujikimu 120K, jumla 360K. Bunge la bajeti litakaa kwa miezi mitatu, akihudhuria vikao vyote atapata 32M, wastani wa 10M kwa mwezi. Kwahiyo hii miezi mitatu ya bunge la bajeti Mbunge ana uhakika wa kukunja 22M kila mwezi.

Sambamba na hayo anapewa mkopo wa 90M kwa ajili ya gari na bima ya afya daraja la kwanza inayomruhusu kutibiwa yeye na familia yake ndani na nje ya nchi. Anapewa lita 1,000 za mafuta kila mwezi.

Vyote hivyo havikatwi kodi. Mtumishi mwenye mshahara wa laki mbili, anakatwa kodi, anakatwa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF/PSSSF), anakatwa bima ya afya, LAKINI Mbunge mwenye karibu 12M kwa mwezi, na marupurupu kibao hachangii chochote kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, hachangii kodi, wala hachangii bima ya afya.

Baada ya miaka mitano, Mbunge huyohuyo anapewa kiinua mgongo cha 240M, ambacho hakuwahi kukatwa kuchangia hata mwezi mmoja. Je pesa hizi za kiinua mgongo anazolipwa zinatoka wapi kama alikua hakatwi? Jibu ni.kwamba zinatoka kwa watanzania maskini including wale wanaolipwa laki mbili kwa mwezi.

Halafu Mbunge mmoja bila aibu anademka eti watanzania walipe tena kodi kwa kutumia simu zao. Yeye anaiita kodi ya uzalendo na ameshauri ilipwe kila siku. Yani kila ukiamka unakatwa kiasi fulani cha pesa kwenye simu yako kama kodi ya uzalendo.

Wabunge walipaswa kuonesha mfano wa uzalendo. Wakatwe kodi kwenye mishahara yao na posho zao zote. Mbunge akiangalia salary slip yake aone Gross salary ni 11.8M lakini Net saalary ni 7M. Akatwe Bima ya afya, akatwe pensheni pia. Hapo atakua na adabu na ataongea lugha moja na wananchi, maana atakua anafeel kile wananchi wake wanafeel.

Na akipoteza ubunge akiwa na miaka 30 asubirie hadi afikishe miaka 60 ndipo apate mafao yake. Wale wanaopoteza ubunge wakiwa na mika zaidi ya 60 ndio wapewe mafao yao kwa wakati. Na wapewe kwa kadri walivyochangia kwenye mifuko ya hifadhi za jamii. Kama alikua anakatwa 500K kwa mwezi kwa ajili ya pensheni means baada ya miaka mitano atakua amechangia 30M. Hiyo ndio haki yake, lakini asipewe hadi afikishe miaka 60.

Hapa ndio tutaona kweli ni wazalendo. Sio wanatunga sheria za kiiimla kukandamiza wanyonge, halafu wao wanajiondoa kwenye sheria hizo. Wanaishi kwenye dunia yao halafu wakishavimbiwa nyama choma na Dompo wine, wanabweka kuhusu uzalendo. Uzalendo gani wakati umezuia fao la kujitoa kwa vijana maskini, while wewe unavuta mshiko kila baada ya miaka mitano?

Unatunga sheria kuwa kijana maskini aliyetoka chuo akapata ka mkataba ka miaka miwili, akimaliza mkataba wake eti asilipwe mafao yake hadi afikishe miaka 60. Lakini wewe ukipoteza ubunge na miaka 35 unataka uvute mafao yako fasta. Hutaki kusubiri ufikishe miaka 60. Huu ndio uzalendo mnaohubiri?

Halafu hawa watanzania unaotaka walipe kodi ya uzalendo kupitia simu zao ni wapi? Hawahawa maskini au kuna wengine? Tanzania ina watumiaji wa simu za mkononi milioni 40. Kati yao watanzania milioni 8 matumizi yao kwenye simu hayafiki TZS 1,000/= kwa mwezi. Yani kuna watanzania milioni 8 ambao ndani ya mwezi mzima hawawezi kutumia "buku" kwenye simu. Hawa ndio wanataka kukamuliwa kodi ya uzalendo na mijitu inayolipwa 12M kwa mwezi. Upumbavu mtupu!
 
Hayo mnayogusa ni masilahi ya wanasiasa kiujumla wao hapo si ccm wala upinzani atakae sapoti.
 
Kwa majukumu ya mbunge, huo ni mshahara mdogo sana. Unajua C7 analipwa shilingi ngapi kwa wiki? Au unajua CEO wa Vodacom Tanzania [emoji1241] alipwa shilingi ngapi? Kwa kazi na majukumu ya mbunge na idadi ya watu anaowawakilisha huo ni mshahara pamoja na posho ni kiasi kidogo sana. Ukienda kwenye makampuni ya private yanayofanya vizuri kimapato, mshahara wa shs sijui 4M ni mshahara wa maofisa wa kati kabisa.
we ndo umehama reli mazma sasa. unadiriki vip kulinganisha private sector na serkali inayoish kwa pesa zinazotokana sekta binafs zaid? usisahau serkali haizalishi, inakusanya kodi.

pia hapa hoja si malipo kuwa makubwa bali ni uwiano wa malipo yenyewe kwa nguvu ya kiuchumi kama taifa(keki ya taifa). labda kama ubinafs si tatzo kubwa kwako! kazi za mbunge zinajulikana mkuu.

Ndo mana hata la saba wamo! gharama nyingine ni za kujitakia kwa kuendekeza mfumo mbovu wa rushwa na kulazimisha ushawish hasa kama hustahili. ndo mana kuna mfuko za jimbo. hili suala halihitaj kujadiliwa kisiasa bali ki haki katika usawa.
 
Pamoja na hayo mkuu wabunge huchangia pesa nyingi kwenye majimbo yao kuanzia misiba,wenye shida mbalimbali sasa unadhani hiyo michango mikubwa bila hiyo pesa wataiweza, labda utakuwa huishi kwenye majimbo yaliyo nje ya Darisalama,kama ungekuwa huku vijijini ungeona jinsi wabunge wanavyotoa michango yao kwenye shughuli nyingi za wapiga kura wao, naamini pia kama una uwezo watu wanaokupiga mizinga kila siku ni wengi ,huyu atakuomba hiki na mwingine kile. Watu wengi wanaolaumu ndio hao hao kila siku wamekuwa ombaomba kwa watu wenye vipato wakiwemo wabunge.
tabia ya kutoa misaada itungiwe sera na sheria mpya mana ni tabia ya ki rushwa rushwa. ilibid wananchi ndo wawe na morali ya kumchangia mbunge kutimiza majukum yake kwa faida yao. usihalalishe huku kujipendekeza kwa wabunge wasiostahili kuongoza wakaishia kuhalalisha kutupiga makusanyo yetu kibunge. kuna kitu kimejengeka kwa wananchi (virus) kuhusu majukum ya mbunge kias kwamba hata kutoa msaada nje ya mfuko wa jimbo linageuzwa jukum lake. hii ni aina ya rushwa na inatutafuna katika marejesho kwa mtoaj.
 
Kutana na #MALISA GJ

UPUMBAVU ni nini? Upumbavu ni huu. Mbunge analipwa mshahara wa 3.8M kwa mwezi, anapata posho 8M kila mwezi, jumla 11.8M. Akiwa kwenye kikao analipwa posho ya kikao 240K kwa siku na posho ya kujikimu 120K, jumla 360K. Bunge la bajeti litakaa kwa miezi mitatu, akihudhuria vikao vyote atapata 32M, wastani wa 10M kwa mwezi. Kwahiyo hii miezi mitatu ya bunge la bajeti Mbunge ana uhakika wa kukunja 22M kila mwezi.

Sambamba na hayo anapewa mkopo wa 90M kwa ajili ya gari na bima ya afya daraja la kwanza inayomruhusu kutibiwa yeye na familia yake ndani na nje ya nchi. Anapewa lita 1,000 za mafuta kila mwezi.

Vyote hivyo havikatwi kodi. Mtumishi mwenye mshahara wa laki mbili, anakatwa kodi, anakatwa mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF/PSSSF), anakatwa bima ya afya, LAKINI Mbunge mwenye karibu 12M kwa mwezi, na marupurupu kibao hachangii chochote kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, hachangii kodi, wala hachangii bima ya afya.

Baada ya miaka mitano, Mbunge huyohuyo anapewa kiinua mgongo cha 240M, ambacho hakuwahi kukatwa kuchangia hata mwezi mmoja. Je pesa hizi za kiinua mgongo anazolipwa zinatoka wapi kama alikua hakatwi? Jibu ni.kwamba zinatoka kwa watanzania maskini including wale wanaolipwa laki mbili kwa mwezi.

Halafu Mbunge mmoja bila aibu anademka eti watanzania walipe tena kodi kwa kutumia simu zao. Yeye anaiita kodi ya uzalendo na ameshauri ilipwe kila siku. Yani kila ukiamka unakatwa kiasi fulani cha pesa kwenye simu yako kama kodi ya uzalendo.

Wabunge walipaswa kuonesha mfano wa uzalendo. Wakatwe kodi kwenye mishahara yao na posho zao zote. Mbunge akiangalia salary slip yake aone Gross salary ni 11.8M lakini Net saalary ni 7M. Akatwe Bima ya afya, akatwe pensheni pia. Hapo atakua na adabu na ataongea lugha moja na wananchi, maana atakua anafeel kile wananchi wake wanafeel.

Na akipoteza ubunge akiwa na miaka 30 asubirie hadi afikishe miaka 60 ndipo apate mafao yake. Wale wanaopoteza ubunge wakiwa na mika zaidi ya 60 ndio wapewe mafao yao kwa wakati. Na wapewe kwa kadri walivyochangia kwenye mifuko ya hifadhi za jamii. Kama alikua anakatwa 500K kwa mwezi kwa ajili ya pensheni means baada ya miaka mitano atakua amechangia 30M. Hiyo ndio haki yake, lakini asipewe hadi afikishe miaka 60.

Hu undo uzalendo tunaoutaka kwao. Sio wanatutungia sheria za kipumbavu, halafu wao wanajiondoa kwenye sheria hizo. Wanakua na dunia yao halafu wakishavimbiwa nyama choma na Dompo wine, wanabweka kuhusu uzalendo. Uzalendo gani wakati umezuia fao la kujitoa kwa vijana maskini, while wewe unavuta mshiko kila baada ya miaka mitano?

Halafu hawa watanzania unaotaka walipe kodi ya uzalendo kupitia simu zao ni wapi? Hawahawa maskini au kuna wengine? Tanzania ina watumiaji wa simu za mkononi milioni 40. Kati yao watanzania milioni 8 matumizi yao kwenye simu hayafiki TZS 1,000/= kwa mwezi. Yani kuna watanzania milioni 8 ambao ndani ya mwezi mzima hawawezi kutumia "buku" kwenye simu. Hawa ndio wanataka kukamuliwa kodi ya uzalendo na mijitu inayolipwa 12M kwa mwezi. Upumbavu mtupu.!

#MalisaGJ
C&P
 
Moderators naomba huu uzi,uwe stick thread juu pale,ili liwe tangazo kwa hawa wachezea Kodi zetu kwa kivuli Cha uheshimiwa.
Mwalimu mshahara wa laki3 alipe Kodi afu wao wanazingua mshahara mil 10😲😲
 
Moderators naomba huu uzi,uwe stick thread juu pale,ili liwe tangazo kwa hawa wachezea Kodi zetu kwa kivuli Cha uheshimiwa.
Mwalimu mshahara wa laki3 alipe Kodi afu wao wanazingua mshahara mil 10😲😲
 
Back
Top Bottom