Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
"Kuna mpango gani wa kuongeza posho kwa Askari na Maafisa Waandamizi wa uchaguzi" - Mhe. Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja
"Wakati wa uchaguzi wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kwa ngazi ya Jimbo na Kata hulipwa posho za kujikimu wanapokuwa wanatekeleza majukumu ya uchaguzi kwa kuzingatia waraka wa Utumishi wa Umma kuhusiana na posho za Serikali" - Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
"Serikali imefanya maboresho kwa kuongeza viwango vya posho kupitia waraka wa Utumishi wa Umma No. 1 uliotolewa tarehe 24 Mei, 2022. Watendaji na walinzi wa vituo vya kupigia kura utaratibu wa kuboresha viwango vyao vya posho utazingitia Wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na bajeti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025" - Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
"Uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura utaenda sambamba na uboreshaji wa posho kwa mwaka 2025. Mwaka huu 2024 tuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao ni uchaguzi wa kwanza kwa awamu ya sita. Je, hawaoni kuna haja ya kuanza kulipa posho mwaka huu ili iweze kuleta Motisha katika chaguzi?" - Mhe. Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja
"Zanzibar, Maafisa Usimamizi wa Uchaguzi na Askari huwa wanasimamia chaguzi mbili tofauti. Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Tanzania na Wabunge wa Bunge la Muungano na Uchaguzi wa kumchagua Rais wa Zanzibar na Wawakilishi na Madiwani Zanzibar. Je, hawaoni kuna umuhimu wa kulipa posho mbili" - Mhe. Angelina Adam Malembeka, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja
"Waraka wa Utumishi wa Umma No. 1 mwezi Mei 2022 tayari umeanza kutumika. Zingatio la kulipa posho lipo. Maboresho yatafanyika Tume ya Uchaguzi itakapokaa kufanya tathmini pamoja na kupitisha bajeti ya uchaguzi mwaka huu 2024" - Mhe. Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu