Mbunge Assa Makanika: Wananchi changamkieni fursa za matibabu ya bure

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE ASSA MAKANIKA: WANANCHI CHANGAMKIENI FURSA ZA MATIBABU YA BURE

WANANCHI KIGOMA WAPATA MATIBABU BURE

Madaktari Bingwa 11 kutoka nchini China πŸ‡¨πŸ‡³ wameweka kambi ya Siku 5 katika Halmashauri ya Kigoma ili kutoa matibabu ya bure kwa wananchi wa Kigoma na kutoa huduma za upasuaji na Masuala ya Mifupa ambapo watu takribani 15,000 wamekusudiwa kufikiwa.

Madaktari Bingwa hao wamepokelewa katika Kata ya Kalinzi Jimbo la Kigoma Kaskazini wakiongozwa na Balozi wa China πŸ‡¨πŸ‡³ hapa nchini Mhe .Chen Mingjian na kupokelewa na wananchi ambalo liliandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Mhe. Assa Makanika.

"Watasaidia kutoa huduma bila malipo na kupunguza ulemavu au vifo ambavyo vingeweza kutokea katika jamii yetu. Ni msaada mkubwa siyo tu Kigoma Kaskazini lakini kwa Mkoa mzima" - Jesca Leba, Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma

"Kwa siku ya kwanza madaktari Bingwa wameanza kuhudumia watu 270 ikiwa ni pamoja na upasuaji mkubwa ambao umefanyika kwa watoto na baadhi ya watu wazima. Nilitegemea nitagusa watu wa Kigoma Kaskazini kupitia huduma lakini matokeo yake tumegusa na Wilaya jirani na Wilaya ya Kigoma Vijijini" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Watu kutokea Wilaya jirani kama Wilaya ya Buhigwe na Wilaya ya Kasulu walikuwepo kwenye kituo cha Afya cha Bitale. Jambo hili kubwa kwa Mashirikiano makubwa tumeweza kulichakata na limeleta Matunda makubwa kwa Mkoa wa Kigoma" - Mhe. Assa Makanika, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini

"Wote tunajua, China πŸ‡¨πŸ‡³ na Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ tunafurahia mahusiano yetu tangua karne zilizopita. Napenda kuwa muwazi, mahusiano binafsi (Personal Relationship) kati yangu na Mbunge Makanika yamechangia kwa kiasi kikubwa kufanikiwa. Ninasisitiza, China πŸ‡¨πŸ‡³ itaendeleza mahusiano na Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ" - Mhe. Balozi Chen Mingjian, Balozi wa China nchini Tanzania.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…