Mbunge Bahati Ndingo Aishinikiza Serikali Kuharakisha Fidia kwa Wananchi Walioathiriwa na Upanuzi wa Hifadhi

Mbunge Bahati Ndingo Aishinikiza Serikali Kuharakisha Fidia kwa Wananchi Walioathiriwa na Upanuzi wa Hifadhi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mbunge wa Mbarali, Bahati Ndingo, ameitaka serikali kuharakisha malipo ya fidia kwa wananchi wa jimbo lake walioathiriwa na upanuzi wa mipaka ya hifadhi ulioingia kwenye maeneo yao.

Akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii bungeni Dodoma, Ndingo amesema mchakato wa fidia kwa wananchi hao umekuwa ukichukua muda mrefu, huku baadhi wakisubiri hadi miaka mitatu bila kupatiwa stahiki zao.

Kutokana na hali hiyo, ameshauri serikali kuwaruhusu wananchi hao kuendelea na shughuli zao kwa utaratibu maalum na uangalizi, ili kuepusha migogoro wakati wakisubiri kukamilika kwa taratibu za fidia.
 
Back
Top Bottom