Mbunge Bengi Mazana: Bajeti ya 2026/2027 nafasi za uongozi Wanawake haifiki asilimi 30, wapo wengi wenye uwezo

Mbunge Bengi Mazana: Bajeti ya 2026/2027 nafasi za uongozi Wanawake haifiki asilimi 30, wapo wengi wenye uwezo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mbunge wa Viti Maalum, Beng'i Mazana Issa akichangia Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka 2026/2027 Bungeni leo Juni 22, 2026 amependekeza Serikali kuangalia uhusishwaji wa Wanawake kwenye nyanya mbalimbali za uongozi akirejelea kuwa Bajeti kuu imetaja nafasi za uongozi kwa Wanawake kwa asilimia 30

"Lakini ningependa kutoa mapendekezo. Nilivyoangalia ile bajeti, kwenye nafasi za uongozi wa wanawake, wanawake hawafiki asilimia 30 katika ngazi zote, kuanzia ngazi za juu, ngazi za kati mpaka ngazi za chini. Na hii inaweza ikafanyiwa kazi vizuri tu kama wizara, hasa ofisi ya Rais mipango, kama italichukulia hili swala kwa uzito. Kwa mfano, sisi ambao tumefanya kazi serikalini tunafahamu kwamba unapokuwa kwenye bodi, mwanamke akiwekwa mmoja kwenye bodi inaonekana ndo tayari wameweka wanawake.

Wanawake ambao wana uwezo wapo wengi tu na tungeangalia kwenye hizi bodi tuongeze idadi ya wanawake, wanawake wakae hata watatu."

'
 
Duh wanawake wenyewe ndiyo hawa waliofanya yao Oct 29,?
 
Back
Top Bottom