Kuna mambo yanayoamuliwa hapa nyumbani yafanyike, ni kwa ajili ya familia yetu. Lakini angalizo kabla yakuamua tujiulize vipaumbele vyetu ni vipi? Je ni wakati sahihi? Tunafanya haya kwa mihemko au ni kwa manufaa ya wote?
Kila Siku wale jamaa wa ng'ambo wanavyotuangalia wanatuona kama watoto wakati mwingine...Planning ni muhimu lakini pia tufanye vitu kitaalam katika dunia ya leo. Kuanzisha biashara au mradi katika level ya Familia hii kubwa halafu mwisho wa siku tija yake inakuja kuoneka ni ndogo sanaaa kwa kweli si tuu unawaumiza wanafamilia lakini unaifanya familia idharaulike.
Haya tunarudi kule kule kuna wanafamilia ni wabobevu wa mipango mbalimbali, wataalamu wa biashara, wataalam wa mikakati katika maendeleo ya miji, vijiji, n.k.
Jamani umri wa hii familia ni mkubwa sanaa tufanye vitu kitaalam bila kujali huyu mtaalam amepinda put au anakengeza, mfupi, mweusi, ili mradi utaalam wake utaleta tija kwenye familia tumtumie kwa wakati huu ndiyo maana Mungu aliruhusu tumbo la mama yake limbebe miezi yote tisa na kuzaliwa kwenye makazi ya familia hii.
Hakuna mwanafamilia aliyepo hapa kihasarahasara.