Bunge hili lina hadhi yoyote ambayo unaweza kusema linatakiwa kuilinda? Kwangu mimi naliona ni kama genge la wahuni walioamua kuvaa suti. Hiyo suruali ya huyo dada inaweza kuzidi uovu:
1) wa spika kumtandika rungu mwenzake mpaka kuzimia, na kisha kumwomba mwendazake amteue kuwa DC ili kupunguza ushindani?
2) wa spika kula njama na mahela ya kumwengua mgombea wa upinzani ili apite bila kupingwa?
3) wa robo tatu yao kuwa wateule wa marehemu na siyo wachaguliwa wa wanachi. Robo taru yao, wote siyo wale walioongoza kwenye kura za maoni
4) wa karibia wote kuwa zao la maagizo ya ibilisi kuwa lazima watangazwe washindi?
Mambo makubwa mawili, dhuluma na mauaji, ni lazima yalete laana. Wabunge hawa, kama alivyokuwa kiongozi wao, wamelaanika, wanatembea na kuishi na laana mpaka vizazi vyao vya nne kwa sababu ni mazao ya dhuluma.