Tukio la leo asubuhi , lalamiko la Mbunge wa Nyangw'ale Hussein Nassor Amar akilalamika ati Mbungwe mwenziwe Condester Minael Sichalwe kavaa visivyo, limeelezea zaidi mtoa hoja anafikiri nini huko Bungeni kuliko kile “waliomchagua” kuwawakilisha wanachokitaka toka kwake.
Tunaifahamu Dodoma, na jinsi watu wanakaa bila wake zao kwa muda mrefu, na tunafahamu imagination ile Mbunge kama huyu wa Nyang’wale anavyoweza kufadhaika kiakili pasipo na sababu.
BINTI YULE ALIVAA VIZURI KABISA.
View attachment 1805304
Tena kwa heshima kabisa, sasa sijui huyu Hussein Nassor Amar alitaka avae baibui au?
Hata picha zinaonhesha binti yuko sawa kabisa.
Mbunge wa Nyang’wale alipita ubunge kwa vigezo vipi haswa vya kutetea chama na maslahi ya nchi?