Mbunge Deo Sanga wa Makambako afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu

Mbunge Deo Sanga wa Makambako afunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu

Mkuu Maulaga59, hapa nazuia nini na we we unafanya nini kuhusu the right to privacy?. Ila pia kasema ukweli, umbea mwingine...., mimi niko very open kuhusu maisha yangu both public life as well as private life, Enyi Waume Wapendeni Wake Zenu!-Wife Kanirudia Saa12:00 Asubuhi!-Bado Nampenda! humu nilisema kila kitu!.

Kina vitu vingine vinatutokea kwenye maisha yetu unakuta sio sisi ni shetani!. Kwa taarifa yako hiyo dada wala hakuwa a house girl!, ni mdada tuu mwenye kazi yake mzee mzima nikafika bei, nikamuachisha kazi na nikavuta jumla!.

Mastori ya Pasco.



Hivyo mtu anayeitwa house girl ni titles tuu, baadhi ya ma house girls ni zaidi ya ma housewife kwenye yale mengineyo!. Unadhani kule kuna alama mama grades kuwa hiyo ni ya housewife ,hiyo ni ya house girl na hii ni wale madanga!, the services are all the same and sometimes more or less!. Tusiwadharau kabisa beki 3!, wanaokoa sana majahazi kwa kuwasaidia sana wale wamama wenye nyumba ambao ni wavivu wavivu!.

P
Mchango wa leo sijauunga mkono kabisa lakini paragraph ya mwisho kwenye hii post yako niliyoi-quote hapa nakubaliana nayo kwa asilimia zote.
 
Deo Sanga maarufu kama Jah People ambaye ni mbunge wa Jimbo la Makambako, leo 14/9/2022 amefunga ndoa Takatifu katika Kanisa Katoliki mjini humo .

Chanzo: Mwananchi

View attachment 2357168

=====
Mbunge wa Makambako mkoani Njombe, Deo Sanga maarufu ‘Jah People’ amefunga ndoa na mkewe Suzana Kapasi leo Septemba 14, 2022 katika kanisa Katoliki Ilangamoto, Makambako Njombe.

Baada ya ndoa hiyo, hivi sasa sherehe ziliendelea katika uwanja wa mpira wa miguu wa Amani ambapo Viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo, Waziri wa Maliasili na Utali, Dk Pindi Chana.

Wengine ni wabunge mbalimbali akiwemo William Lukuvi (Isimani-Iringa), Festo Sanga (Makete) na Joseph Kamonga (Ludewa) pamoja na wananchi wa Mji wa Makambako.

Padri Ladislaus Mgaya wa Jimbo la Katoliki Njombe ndiye aliyewafungisha ndoa hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Jah people zile lori ni zake au kajipa tu ilo jina
 
Naomba tujifunze kuheshimu the right to privacy ya haki za faragha za watu!.

Mtu kuoa au kuolewa ni issue private ya maisha binafsi ya mtu, kama mtu anapoamua kukaa bar au kustarehe popote, hiyo ni haki binafsi ya faragha, haki hiyo inabidi iheshimiwe, unless kama ni yeye mwenyewe amealika media akawaruhusu mtangazie dunia kuwa ameoa!.
P
Hata kupata kura 1 kule Kigamboni na kukatwa kwenye Bunge la Afrika Mashariki ni haki yako.
 
Kupitia taarifa hii rasmi naamini kuwa Kuna taarifa nyingi huwa tunalishwa matangopori.Huyo mwanamke ni wa kitambo mno ila vile tu wakati imewapendeza wabariki ndoa yao.Acheni kudanganyana hapa.

Posting from MAKAMBAKO.
 
It is not true, uandishi wa habari pia una maeneo maeneo tofauti tofauti, enzi zangu wakati naanza uandishi wa habari, Tanzania tulikuwa na main stream media only, redio ilikuwa moja RTD na magazeti mawili ya dailies, Daily News/Sunday News na Uhuru/Mzalendo na one weekly Mfanyakazi, hakukuwa na tabloids za udaku. Mwinyi ndio amefungua rukhsa na media boom kwa kuruhusu private media na ndipo magazeti ya udaku yakaibuka na kuchipukia ila mimi sikuwahi kuandika udaku wowote.

Kitu nilichokuwa nafanya mimi ni kuandika IJ, kwenye kuandika IJ hakuna jinsi ni lazima ulipue watu na kuumiza watu, hivyo kwenye hili, kiukweli nimelipua wengi, nimetesa wengi, na kulipua mabomu mengi, matokeo yake, nimekuja kufidia kupitia karma.

P
Basi tambua habari ya ndoa haina ubaya. Ingelikuwa kakutwa na mchepuko hapo saawa
 
Naomba tujifunze kuheshimu the right to privacy ya haki za faragha za watu!.

Mtu kuoa au kuolewa ni issue private ya maisha binafsi ya mtu, kama mtu anapoamua kukaa bar au kustarehe popote, hiyo ni haki binafsi ya faragha, haki hiyo inabidi iheshimiwe, unless kama ni yeye mwenyewe amealika media akawaruhusu mtangazie dunia kuwa ameoa!.
P
Ndoa sio ishu private.

Ni jambo la kijamii ndio maana linafanyika in an open space , kunakuwa na tangazo la ndoa na cheti kinasajiliwa serikalini.

Na mwanandoa anawekwa alama kidoleni ili jamii yote ijue kuwa kaoa au kaolewa.
 
Ndoa sio ishu private.

Ni jambo la kijamii ndio maana linafanyika in an open space , kunakuwa na tangazo la ndoa na cheti kinasajiliwa serikalini.

Na mwanandoa anawekwa alama kidoleni ili jamii yote ijue kuwa kaoa au kaolewa.
Kwenye the right to privacy, Tanzania bado tuna safari ndefu sana!. Japo harusi ni tukio la public linafanyika bila kificho kama mtu anavyoingia hotelini kula au club kufurahi, mambo binafsi ya mtu, yanalindwa na kinga ya the right to privacy hata kama yamefanywa public. Huwezi kuchukua picha ya harusi ya mtu na kuposti in public bila ridhaa ya mhusika, its an invasion of privacy function.
NB. Dalili zote za tukio hili zina suggest wahusika waliridhia, ila pia kama lengo ni kuonyesha furaha ya harusi, zile picha alipaswa kupigwa soap soap kwenye photoshop angalau kumsoap soap Bi Harusi!. Tasnia yetu ya sheria Tanzania ingekuwa inaruhusu probono za civil litigation, hapo nakula pesa nje nje ya defamation by innuendo!.
P
 
Back
Top Bottom