Mbunge Edward Ole Lekaita Atoa Darasa la Sheria Kuhusu Kutatua Migogoro ya Ardhi Nchini

Mbunge Edward Ole Lekaita Atoa Darasa la Sheria Kuhusu Kutatua Migogoro ya Ardhi Nchini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MBUNGE EDWARD OLE LEKAITA ATOA DARASA LA SHERIA KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI NCHINI

"Mhe. Jerry Silaa tangu umeteuliwa umefanya kazi kubwa hasa kupitia Kliniki ya Ardhi, endelea hivyo hivyo kwani matarajio ya Mheshimiwa Rais na wananchi walio wengi wanataka migogoro ya Ardhi iishe na tuwasikilize wananchi" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto

"Ombi nililonalo ni kuwa Kiteto tunamtaka Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya mtuletee kwa haraka sana, Kiteto ni kubwa, migogoro ni mingi. Mkituletea Mwenyekiti wa kututembelea siyo sawa"

"Migogoro ya Ardhi ni dhana kubwa, Ardhi ni uhai, Ardhi ni mali, Ardhi ni tamaduni za watu na maisha ya watu. Inahitaji utulivu, umakini, weledi mkubwa sana, utawala wa sheria, na sheria itafsiriwe kama ilivyotakiwa na Bunge na inahitaji teknolojia kwasababu nchi yetu ni kubwa kupima, kupanga kwa teknolojia nzuri ambayo haitengenezi migogoro"

"Migogoro mingi ya Ardhi tuliyonayo, kila ukituma wataalamu kwenye eneo inatengeneza ramani yake, unaweza kukuta mgogoro mmoja una ramani sita. Fedha zimetumika za Serikali lakini watalaam wetu wa Ardhi wanatuangusha sana"

"Naamini utalamu walionao wataalam wetu wa Ardhi ni wa kusoma GPS, Kutumia mashine na kusoma Sera na Sheria ya Ardhi lakini siyo wataalam wa mapori ya wananchi. Ni lazima kushirikisha wananchi, ni jambo muhimu mno kuwasikiliza wenyeji wa eneo"

"Ili kuondokana na migogoro ya Ardhi ni lazima tuwe na Tume ya Matumizi bora ya Ardhi yenye bajeti kubwa sana. Kati ya Vijiji 12,318 itakuwa ni vijiji 4126 vitakuwa na matumizi bora ya Ardhi. Kuna vijiji zaidi ya 8192 visipopata majawabu migogoro haitakaa iishe"

"Tuamue, kama tunataka kumaliza migogoro ni lazima Tume ya Matumizi bora ya Ardhi iwe na fedha nyingi sana. Tupime vijiji kwanza, tukishamaliza vijiji vikawa na hati na matumizi bora ya Ardhi tutakwenda kwenye Ardhi binafsi baada ya vijiji kufahamika mipaka yake"

"Tanzania Ardhi imegawanyika katika sehemu tatu; Ardhi ya Vijiji, Ardhi ya hifadhi na Ardhi ya jumla. Ardhi ya vijiji ilikuwa ni 70%, Ardhi ya hifadhi ilikuwa ni 28% na ardhi ya jumla ilikuwa ni 2% lakini sasa hivi imekuwa ni kinyume"

"Kuna aina tano za kutambua ardhi ya vijiji; Kama Kijiji kina hati na kimepimwa, Kijiji kilichoanzishwa kwa Operesheni vijiji, Kijiji ambacho wananchi wamekuwa wanakaa tu, Ardhi ambayo vijiji vimekubaliana, ardhi ambayo wananchi wanaishi kwa maisha ya kijijini kwa zaidi ya miaka 12. Popote wanapoishi wananchi sasa ni ardhi ya vijiji iwe wana hati au hawana kwa mujibu wa sheria"

"Linapokuja suala la Ardhi, Waziri wa Ardhi ndiyo mkubwa kuliko Waziri yeyote. Unatakiwa ututafsirie Ardhi ya kijiji ni wapi, ya hifadhi ni wapi na Ardhi ya jumla ni wapi. Ukiona watu wa Maliasili wanakuja kugombana na Wananchi ujue hamfuati Sheria. Watu wa maliasili walitakiwa waje kwa Waziri wa Ardhi waombe uwape mipaka ya vijiji inapoishia"

"Kiteto tumekuwa na mgogoro wa muda mrefu kati ya Manyara na Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ardhi na Takwimu mwaka 2015 imetengeneza ripoti ya tathimini na mipaka mkatuchorea ramani ya vijiji na hati mkatupa baada ya miaka mitatu wanakua wengine wanasema wale walikosea, sasa twende wapi?"

"Mgogoro mmoja wa Ardhi unakuwa na ramani sita mpaka saba, mnawachanganya wananchi pasipokuwa na sababu za msingi. Hiyo muache. Waziri wa Ardhi naomba uje, tunachotaka ni tafsiri sahihi ya ramani ya Mkoa wa Manyara na Mkoa wa Dodoma, tunahitaji vifaa ambavyo ni sahihi kwaajili ya kupima Ardhi kwa usahihi"

"Ramani ya mgogoro wa Ardhi ya mpaka wa Manyara na Dodoma kuna michoro zaidi ya mitatu, na Tume tatu kila mtu ana ramani yake, hapo mwananchi atakwenda wapi. Migogoro ipo kwa sababu wananchi hawashiriki. Mgogoro wa Manyara na Tanga (Kilindi) msimamie vizuri ili migogoro iishe" - Mhe. Edward Ole Lekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto
 

Attachments

  • BUNGE MAY 24 MHE EDWARD.mp4
    66.7 MB
Back
Top Bottom