Mbunge Fransic Mtinga: Serikali ilijidanganya kupandisha bei ya kuunganishia umeme, ataka irudishwe kuwa Tsh. 27,000

Mbunge Fransic Mtinga: Serikali ilijidanganya kupandisha bei ya kuunganishia umeme, ataka irudishwe kuwa Tsh. 27,000

Nafikiri wizara ya nishati na Tanesco haziko mikononi mwa watu sahihi wameshindwa kufikiria vizuri juu ya kadhia ya bei ya kuunganishiwa umeme hapo awali mbona iliwezekana kuunganishiwa kwa bei ya chini sio lazima iwe kama ile ya awali (27,000) lakini ishuke wengi waweze kuimudu maana wataendelea kununua luku kila iitwayo siku.
 
Dodoma. Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Fransic Mtinga ametaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuweka gharama za kuunganisha umeme kwa Sh27, 000 kote nchini ili kukusanya makusanyo mengi kutokana na mauzo ya umeme na kodi ya majengo.

Ameyasema hayo leo Jumatano Mei 31, 2023 wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24.

Amesema Tanesco inafanya biashara kwenye kuuza umeme na kuunganisha umeme kwasababu wanatoza Sh320, 000 kwa maunganisho ya umeme mijini.

Amesema wanaounganisha umeme kwa kiasi hicho mijini, ni ndogo na kwamba wakati gharama zilipokuwa Sh27, 000 wateja walikuwa ni wengi sana.

“Kipindi ambacho ilitangazwa umeme uwekwe kwa Sh27000 maombi ya kuunganishiwa umeme yalijaa Tanesco hadi wakashindwa kufanya kazi lakini watu hawa ni wa mjini,”amesema.

Amesema watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme na hivyo anaona fursa hiyo wameiacha ya kukusanya mapato mengi.

Mtinga amesema bora wangeweka Sh 27,000 kama gharama ya maunganisho kwa watu wote lakini baada ya muda mfupi watu wengi wakatumia umeme.

Amesema hatua hiyo itawafanya Tanesco kuingiza mapato kwasababu watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme.

“Kama tunaweza kupeleka umeme zaidi ya kilometa 200 toka kijiji kimoja hadi kingine kwa gharama za Serikali na kwamba wataunganisha kaya 15 hadi 20. Kuna maeneo ambayo nguzo moja inaweza kubeba hadi mita 15,” amesema.

Amesema kwa Sh27, 000 zitawawezesha watu wengi kuanganisha umeme na Tanesco ikapata fedha kutokana na ununuzi wa umeme kuliko kuwawekea Sh320, 000 halafu hawavuti umeme.

Amesema kwanini wasitumie fursa kwa kukusanya kodi ya majengo ya Sh12, 000 kwa mwezi kila mita na kwamba wanaweza kuongeza mapato ya Serikali.
Aweke takwimu sio anaongea tuu
Haya ndio madhara ya kukosa akili,aangalie population pattern then atakuwa tuna kaya ngapi wapi na Zina uwezo gani kiuchumi

Kuongea tuu Kwa hisia bila ushahidi wa takwimu ni upuuzi
 
Wewe umetoa takwimu ipi
Mimi nasimama na Tanesco Kwa sababu hata bei ya Sasa ya 320,000 ni bei ya ruzuku sio ya soko Sasa kupunguza zaidi ni kuua shirika.

27,000 Bado Iko Vijijini lakini hakuna wanaoongiza umeme Kwa Kasi
 
Kwanini punguani matumizi ya luku ni endelevu kwanini ushauri huo usifatwe bei ya kuunganisha umeme ikashuka ili kuwa na maombi mengi zaidi na watumiaji wengi zaidi wa luku kuliko kuwa na bei kubwa wachache wenye kuzimudu chukulia mfano wa kampuni za simu hasa kwenye huduma za fiber internet zinalazimika kuingia harama kubwa ya kuweka miundombinu lakini mteja halipii hizo gharama

Wewe umetoa takwimu ipi
Ulishawahi bila shaka hujawahi kufanya utafiti?
 
Mimi nasimama na Tanesco Kwa sababu hata bei ya Sasa ya 320,000 ni bei ya ruzuku sio ya soko Sasa kupunguza zaidi ni kuua shirika.

27,000 Bado Iko Vijijini lakini hakuna wanaoongiza umeme Kwa Kasi
Ile ni biashara why nilipie vifaa kama nguzo na nyaya alafu watu wengine waunganishiwe huduma na miundombinu iwe yao. Huo ni wizi wao kazi yao ni nini.
 
Ile ni biashara why nilipie vifaa kama nguzo na nyaya alafu watu wengine waunganishiwe huduma na miundombinu iwe yao. Huo ni wizi wao kazi yao ni nini.
Hakuna anaelipia hivyo vitu saizi,unaomba umeme unalipa 320,000 ndani ya Siku 4 umeme unawaka.

Mwisho ukisema Kwa nini ulipie Sasa sijui wanaopanga bei za vitu Huwa wanaopanga ulipie nini kama sio gharama za uzalishaji na faida Juu?
 
Maandamano ya nchi nzima yanahitajika kuishinikiza hii serikali iwe ni yenye tija kwa wananchi na si kwa watu wachache.
Niandamane wakati tayari nina umeme?

Waandamane ambao hawana umeme
 
Hakuna anaelipia hivyo vitu saizi,unaomba umeme unalipa 320,000 ndani ya Siku 4 umeme unawaka.

Mwisho ukisema Kwa nini ulipie Sasa sijui wanaopanga bei za vitu Huwa wanaopanga ulipie nini kama sio gharama za uzalishaji na faida Juu?
Hiyo ni gharama kama hawataweka nguzo, maana yake uko umbali wa mita hamsini kutoka nguzo ilipo. Zaidi ya hapo jiandae kulipa mamilioni ndo upate huo umeme
 
Hiyo ni gharama kama hawataweka nguzo, maana yake uko umbali wa mita hamsini kutoka nguzo ilipo. Zaidi ya hapo jiandae kulipa mamilioni ndo upate huo umeme
Ni kweli ila Mkiwa wengi Nje ya huo umbali hamlipii ila Ukiwa mwenyewe utachangia Kwa sababu wanasema ku mservice mtu mmja is too expensive.
 
Ni kweli ila Mkiwa wengi Nje ya huo umbali hamlipii ila Ukiwa mwenyewe utachangia Kwa sababu wanasema ku mservice mtu mmja is too expensive.
Hata nyumba zikiwa kumi hawakubali wanataka mjichange msogeze huduma sio kwamba watasema pale ziko nyumba kumi tuwasogezee huduma.
 
Mimi nasimama na Tanesco Kwa sababu hata bei ya Sasa ya 320,000 ni bei ya ruzuku sio ya soko Sasa kupunguza zaidi ni kuua shirika.

27,000 Bado Iko Vijijini lakini hakuna wanaoongiza umeme Kwa Kasi
Unauwaje shirika kwa kuongeza wateja?
 
Back
Top Bottom