Mbunge Fransic Mtinga: Serikali ilijidanganya kupandisha bei ya kuunganishia umeme, ataka irudishwe kuwa Tsh. 27,000

Mbunge Fransic Mtinga: Serikali ilijidanganya kupandisha bei ya kuunganishia umeme, ataka irudishwe kuwa Tsh. 27,000

Kitu nimegundua ni kwamba Mungu alikosea kutuondolea dhahabu akatuachia moram
 
Kuna siku nikapiga simu TANESCO,kuuliza mbona hadi kijijini mnakata kodi za majengo wakanijibu ndo sheria ipo ivo...
 
Aisee! Mbunge kakumbushia jambo la msingi sana. Umeme ni sehemu ya huduma ya jamii, na ni kazi ya serikali kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi wote bila ubaguzi. Umeme siyo anasa karne hii!

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Ilitakiwa uwe bure kabisa. Kuunganisha umeme na maji viwe ni bure, tulipie matumizi sio maunganisho.
 
Dodoma. Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Fransic Mtinga ametaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuweka gharama za kuunganisha umeme kwa Sh27, 000 kote nchini ili kukusanya makusanyo mengi kutokana na mauzo ya umeme na kodi ya majengo.

Ameyasema hayo leo Jumatano Mei 31, 2023 wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24.

Amesema Tanesco inafanya biashara kwenye kuuza umeme na kuunganisha umeme kwasababu wanatoza Sh320, 000 kwa maunganisho ya umeme mijini.

Amesema wanaounganisha umeme kwa kiasi hicho mijini, ni ndogo na kwamba wakati gharama zilipokuwa Sh27, 000 wateja walikuwa ni wengi sana.

“Kipindi ambacho ilitangazwa umeme uwekwe kwa Sh27000 maombi ya kuunganishiwa umeme yalijaa Tanesco hadi wakashindwa kufanya kazi lakini watu hawa ni wa mjini,”amesema.

Amesema watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme na hivyo anaona fursa hiyo wameiacha ya kukusanya mapato mengi.

Mtinga amesema bora wangeweka Sh 27,000 kama gharama ya maunganisho kwa watu wote lakini baada ya muda mfupi watu wengi wakatumia umeme.

Amesema hatua hiyo itawafanya Tanesco kuingiza mapato kwasababu watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme.

“Kama tunaweza kupeleka umeme zaidi ya kilometa 200 toka kijiji kimoja hadi kingine kwa gharama za Serikali na kwamba wataunganisha kaya 15 hadi 20. Kuna maeneo ambayo nguzo moja inaweza kubeba hadi mita 15,” amesema.

Amesema kwa Sh27, 000 zitawawezesha watu wengi kuanganisha umeme na Tanesco ikapata fedha kutokana na ununuzi wa umeme kuliko kuwawekea Sh320, 000 halafu hawavuti umeme.

Amesema kwanini wasitumie fursa kwa kukusanya kodi ya majengo ya Sh12, 000 kwa mwezi kila mita na kwamba wanaweza kuongeza mapato ya Serikali.
Hii ndo akili kubwa wao wanataka warecover gharama kwa kufunga umeme na sio kuuza umeme
 
Ila watanzania wajinga sana. Yani kutoka 27,000/- mpaka 320,000/- halafu watu wameweka makalio chn kama hakuna kilichotokea.
Na wanasifia eti yule aliyekuwa pale alikuwa shetani huyu ndo anafanya kazi nzuri na anaifungua nchi .
 
Mimi nasimama na Tanesco Kwa sababu hata bei ya Sasa ya 320,000 ni bei ya ruzuku sio ya soko Sasa kupunguza zaidi ni kuua shirika.

27,000 Bado Iko Vijijini lakini hakuna wanaoongiza umeme Kwa Kasi
Kwamba unataka kurecover bei ya material ya kuunganisha umeme are you serous
 
Back
Top Bottom