Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilitakiwa uwe bure kabisa. Kuunganisha umeme na maji viwe ni bure, tulipie matumizi sio maunganisho.Aisee! Mbunge kakumbushia jambo la msingi sana. Umeme ni sehemu ya huduma ya jamii, na ni kazi ya serikali kuhakikisha huduma za kijamii zinawafikia wananchi wote bila ubaguzi. Umeme siyo anasa karne hii!
Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
HahahahaCcm Haituvushi
Hii siio hoja, serikali inajenga lami kilomita moja kwa bilion 2, kwa nini tunapita bure?Tanesco Mita moja wanannunua 150,000/...wakupe wewe Kwa 27,000/..halafu foleni inakuwa miezi sita...inageuka zoezi la rushwa kuruka foleni...
Uko sahihi sana, umemjibu kwa akili kubwaHii siio hoja, serikali inajenga lami kilomita moja kwa bilion 2, kwa nini tunapita bure?
Hii ndo akili kubwa wao wanataka warecover gharama kwa kufunga umeme na sio kuuza umemeDodoma. Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Fransic Mtinga ametaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuweka gharama za kuunganisha umeme kwa Sh27, 000 kote nchini ili kukusanya makusanyo mengi kutokana na mauzo ya umeme na kodi ya majengo.
Ameyasema hayo leo Jumatano Mei 31, 2023 wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24.
Amesema Tanesco inafanya biashara kwenye kuuza umeme na kuunganisha umeme kwasababu wanatoza Sh320, 000 kwa maunganisho ya umeme mijini.
Amesema wanaounganisha umeme kwa kiasi hicho mijini, ni ndogo na kwamba wakati gharama zilipokuwa Sh27, 000 wateja walikuwa ni wengi sana.
“Kipindi ambacho ilitangazwa umeme uwekwe kwa Sh27000 maombi ya kuunganishiwa umeme yalijaa Tanesco hadi wakashindwa kufanya kazi lakini watu hawa ni wa mjini,”amesema.
Amesema watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme na hivyo anaona fursa hiyo wameiacha ya kukusanya mapato mengi.
Mtinga amesema bora wangeweka Sh 27,000 kama gharama ya maunganisho kwa watu wote lakini baada ya muda mfupi watu wengi wakatumia umeme.
Amesema hatua hiyo itawafanya Tanesco kuingiza mapato kwasababu watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme.
“Kama tunaweza kupeleka umeme zaidi ya kilometa 200 toka kijiji kimoja hadi kingine kwa gharama za Serikali na kwamba wataunganisha kaya 15 hadi 20. Kuna maeneo ambayo nguzo moja inaweza kubeba hadi mita 15,” amesema.
Amesema kwa Sh27, 000 zitawawezesha watu wengi kuanganisha umeme na Tanesco ikapata fedha kutokana na ununuzi wa umeme kuliko kuwawekea Sh320, 000 halafu hawavuti umeme.
Amesema kwanini wasitumie fursa kwa kukusanya kodi ya majengo ya Sh12, 000 kwa mwezi kila mita na kwamba wanaweza kuongeza mapato ya Serikali.
Na wanasifia eti yule aliyekuwa pale alikuwa shetani huyu ndo anafanya kazi nzuri na anaifungua nchi .Ila watanzania wajinga sana. Yani kutoka 27,000/- mpaka 320,000/- halafu watu wameweka makalio chn kama hakuna kilichotokea.
Kwamba unataka kurecover bei ya material ya kuunganisha umeme are you serousMimi nasimama na Tanesco Kwa sababu hata bei ya Sasa ya 320,000 ni bei ya ruzuku sio ya soko Sasa kupunguza zaidi ni kuua shirika.
27,000 Bado Iko Vijijini lakini hakuna wanaoongiza umeme Kwa Kasi
zenj ni tanzania vijijiniGood point sn, Mbona Zanzibar ni 27,000 au Zanzibar ni kijijini?
True nduguKitu nimegundua ni kwamba Mungu alikosea kutuondolea dhahabu akatuachia moram
[emoji38][emoji38][emoji38]Na wanasifia eti yule aliyekuwa pale alikuwa shetani huyu ndo anafanya kazi nzuri na anaifungua nchi .
Wajinga wakubwa walezenj ni tanzania vijijini
[emoji38][emoji38][emoji38]Wajinga wakubwa wale