Mbunge Fransic Mtinga: Serikali ilijidanganya kupandisha bei ya kuunganishia umeme, ataka irudishwe kuwa Tsh. 27,000

Ila watanzania wajinga sana. Yani kutoka 27,000/- mpaka 320,000/- halafu watu wameweka makalio chn kama hakuna kilichotokea.
Nchi hii watu wake hawana nyongo ,[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Uyo mbunge kaeleza kwa lugha rahisi sana na ukweli mtupu.

ilikua unaunganisha umeme kwa 27,000 na akuna mgao,lakini sasa kuumganishiwa umeme ni laki tatu na mgao juu.
 

MBUNGE FRANSIC MTINGA ATAKA TSH. 27,000 KUUNGANISHIWA UMEME

Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Fransic Mtinga ametaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuweka gharama za kuunganisha umeme kwa Sh27, 000 kote nchini ili kukusanya makusanyo mengi kutokana na mauzo ya umeme na kodi ya majengo.

Ameyasema hayo Jumatano Mei 31, 2023 wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2023/24.

Amesema Tanesco inafanya biashara kwenye kuuza umeme na kuunganisha umeme kwasababu wanatoza Sh320, 000 kwa maunganisho ya umeme mijini.

Amesema wanaounganisha umeme kwa kiasi hicho mijini, ni ndogo na kwamba wakati gharama zilipokuwa Sh27, 000 wateja walikuwa ni wengi sana.

“Kipindi ambacho ilitangazwa umeme uwekwe kwa Sh27000 maombi ya kuunganishiwa umeme yalijaa Tanesco hadi wakashindwa kufanya kazi lakini watu hawa ni wa mjini,”amesema.

Amesema watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme na hivyo anaona fursa hiyo wameiacha ya kukusanya mapato mengi.

Mtinga amesema bora wangeweka Sh 27,000 kama gharama ya maunganisho kwa watu wote lakini baada ya muda mfupi watu wengi wakatumia umeme.

Amesema hatua hiyo itawafanya Tanesco kuingiza mapato kwasababu watu wa mjini wana matumizi makubwa ya umeme.

“Kama tunaweza kupeleka umeme zaidi ya kilometa 200 toka kijiji kimoja hadi kingine kwa gharama za Serikali na kwamba wataunganisha kaya 15 hadi 20. Kuna maeneo ambayo nguzo moja inaweza kubeba hadi mita 15,” amesema.

Amesema kwa Sh27, 000 zitawawezesha watu wengi kuanganisha umeme na Tanesco ikapata fedha kutokana na ununuzi wa umeme kuliko kuwawekea Sh320, 000 halafu hawavuti umeme.

Amesema kwanini wasitumie fursa kwa kukusanya kodi ya majengo ya Sh12, 000 kwa mwezi kila mita na kwamba wanaweza kuongeza mapato ya Serikali.
 

Attachments

  • makato-pic.jpg
    174.8 KB · Views: 4
Aya ya mwisho nadhani alimaanisha Tzs12,000/= kwa mwaka na sio mwezi kama alivyoandika
 
Haya maajabu mwisho ilikuwa kwa awami iliyopita tu
 
Tanesco Mita moja wanannunua 150,000/...wakupe wewe Kwa 27,000/..halafu foleni inakuwa miezi sita...inageuka zoezi la rushwa kuruka foleni...
 
Pia Tanesco hili la kubofya kwenye mita za luku limepitwa na wakati madada wa kazi hawajui kuingia luku mashine zinasumbua.
Tengenezeni vocha za umeme unanua tu kwenye simu umeme uwaka nyumbani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…