PreGE2025 Mbunge Godwin Kunambi: Ahubiri injili ya "HAKI" bungeni. Apinga vyombo vya dola kubambikizia kesi watu. Asema, duniani tunapita tu

PreGE2025 Mbunge Godwin Kunambi: Ahubiri injili ya "HAKI" bungeni. Apinga vyombo vya dola kubambikizia kesi watu. Asema, duniani tunapita tu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Hana lolote mpuuzi tu huyu..
Kwenye ule uchafuzi mkuu wa 2020 Yeye mwenyewe alipita bila kupingwa. Wagombea ubunge wa Chadema na vyama vingine walifanyiwa figisu wakakatwa wote kugombea na akabaki yeye peke yake. kwanini asingepiga hizi kelele wakati ule?
 
Katika kila jamii au kundi Mungu ana watu wake ambao watasimama siku ile ya Hukumu kama mashahidi wakati watakavyokuwa wakijaribu kujitetea.
 
Ni vizuri Spika awe anawaomba wabunge kutoa ushahidi wa wansyoongea sio vizuri kugeuza bunge kuwa kijiwe cha kuropoka chochote bila ushahidi
Hivi hujawahi kumsikia rais Samia mwenyewe akisema polisi wanabambikia watu kesi? Yaani tunaongozwa na watu wa ajabu na wafuasi wao nao ni madebe shinda tu.
 
Atoe ushahidi wa watu waliobambikizwa kesi vinginevyo anapoteza bure muda wa bunge

Ama uwe huna akili kabisa, au uwe shetani mnafiki, ndiyo utasema hakuna wanaobambikiziwa kesi nchi hii. Na kwenye utawala wa huyu bibi tuliye naye, hakika imekuwa balaa zaidi. Hakika ibilisi ameufanya utawala wake kuwa nyumva yake. Ulimbambikizia kesi Mbowe, umeteka na kuwaua wengi, na sasa umembambikizia kesi ya uhaini Lisu.
 
Mungu amzidishie hekima yake na ujasiri wa kuinena kweli ya Mungu wetu.
 
➡Baada ya kumsikiliza huyu m-CCM naanza kuiona roho ya "TOBA" kwa baadhi ya "WASIOJULIKANA". Na binafsi, naiona nuru mbele kidogo tu. Tunaanza kutoka kwenye giza la mauti liitwalo "CCM" lililotufunika kwa miaka 64 sasa...
Wamo wengi sana waTanzania ambao wako CCM, wanaoona kama huyo mmoja wao, lakini hawathubutu kusema lolote hadi hapo genge linaloendesha yote haya litakapokuwa limeondolewa..., utawasikia wengi sana.

Kwa bahati mbaya sana kwetu sote; hilo genge linalo husika na maovu haya yote haliwezi kuacha uovu hadi hapo litakapokuwa limetimiza kazi ya kumbakisha Samia kwenye urais. Kwa hiyo maumivu usifikiri yatapungua kwa kuwepo na hao CCM wanaotambua yote hayo, na wasiweze kufanya lolote kuyazuia.
Kudhibiti hilo genge ni lazima "No Reform, No Election" iwafikie waTanzania wengi, ambao ndio watakaokataa ushetani wa hawa wachache ndani ya CCM kutuvuruga kama nchi.
 
Atoe ushahidi wa watu waliobambikizwa kesi vinginevyo anapoteza bure muda wa bunge
Wakati mwingine uonage aibu kupanua mdomo wako kuhoji au kupinga vitu au mambo ya haki na yaliyo wazi kabisa...!

Kwani ukiukubali ukweli hata kwa siku moja au mara moja tu utapungukiwa ni nini wewe Shotocan na wenzio kina Tlaatlaah kipara kipya au chiembe au Lucas Mwashambwa...?

Hakuna, hamtapungukiwa na chochote zaidi kwamba mtaongeza siku zenu za kuishi na kutozeeka mapema...

Chuki na visasi na tamaa ya vitu vya dunia hii; fedha na kutaka madaraka ya uongozi kwa njia hata haramu za kuteka, kutesa na kuua watu ambayo ndiyo hulka na tabia yenu vijana wa CCM kwa kuwa mmerithi toka kwa baba zenu wachawi, wezi, mafisadi itawafanya mharibu afya zenu, kuzeeka haraka kabla ya umri na kufa vifo vya ajabu ajabu...

Badilikeni vijana. Tumieni akili kufikiri kabla ya kusema ndiyo kwa kila kitu...!!
 
Ni vizuri Spika awe anawaomba wabunge kutoa ushahidi wa wansyoongea sio vizuri kugeuza bunge kuwa kijiwe cha kuropoka chochote bila ushahidi
Mkuu,bado hujaelewa alichoongea? Ile ni rai ushahidi wa nini? Mbona kama unajishuku?
 
Back
Top Bottom