Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,768
- 2,361
Mbunge wetu Kawe Nd Gwajima sasa anafanya kazi ya wananchi.
Kwa muda mrefu sana wananchi wa eneo la Mbezi Jogoo, nyuma ya viwanda vya COTEX, tume,uwa tukisumbuliwa na matapeli kwa miaka mingi.
Watu wako eneo hili toka miaka ya 70 au 80, mimi nipo hapo toka mwanzoni mwa miaka ya 90.
Eneo letu ni la milima na mabonde, na huko nyuma wizara ya ardhi ilipima kama eneo la viwanda.
Wengi waliopewa maeneo hayo ya milima na mabonde waliyakimbia na kwenda kwingine kuliko tambarare zaidi, maeneo ambayo ni bora kwa viwanda.
Katika miaka ya karibuni matapeli kwa kutumia wanasheria na vile vile kwa kuwatumia wanasiasa fulani, wamekuwa wakizunguka zunguka kutaka kuwabomolea wananchi nyumba zao.
Mwanasiasa aliye nyuma ya sakata hili tunasikia ni yule alikuwa mkuu wa mkoa Awamu ya tano.
Wanatafuta maeneo ya bwerere.
Tunamshukuru mbunge Gwajima kwa kuwaleta Waziri Nape na Naibu waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete na kutuhakikishia kuwa eneo hilo hati za viwanda vimefutwa na maeneo yatarasimishwa kwa wananchi.
Huu ni ukombozi, na sasa amani imerudi kwa wananchi wa Mbezi Jogoo.
Tunaishukuru sana Awamu ya Sita chini ya Mama Samia.