Mbunge Hawa Mwaifunga akataa Madawati 48, asema “Mwalimu Nataka Milioni 3 Zangu”

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mbunge wa Tabora Mjini, Hawa Mwaifunga amekataa kupokea madawati 48 yaliyotengenezwa kwa ajili ya shule tatu katika jimbo hilo baada ya kuyakagua na kutoridhishwa na ubora wake, Septemba 18, 2026.

Madawati hayo yaligharimu kiasi cha Shilingi milioni tatu, fedha zilizotolewa kupitia Mfuko wa Jimbo, huku kila dawati likigharimu Shilingi 70,000.

Madawati hayo yaligawanywa kwa shule tatu, ambapo Shule ya Msingi Timkeni ilitengewa madawati 10, Shule ya Msingi Mihama madawati 10 na Shule ya Msingi Mpepo madawati 28.
Madawati hayo yalitengenezwa na Kampuni ya Diget, huku mchakato wa zabuni ukisimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Baada ya kukamilika, Mbunge Hawa Mwaifunga alifanya ukaguzi wa madawati hayo kabla ya kukabidhiwa kwa shule zilizokusudiwa. Hata hivyo, baada ya kuyakagua, hakuridhishwa na ubora wake na kuamua kutoyapokea.

Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo amedai kurejeshewa fedha zilizotumika katika utengenezaji wa madawati hayo, huku akitaka suala la ubora na mchakato wa utekelezaji wa mradi huo kufanyiwa ufafanuzi.

Tukio hilo sasa limeibua maswali kuhusu mchakato wa zabuni, matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo na udhibiti wa ubora wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za umma.
 
Mbona anaongea kama DC?
 
Kihere here tu cha waalimu, Ni kazi ya mwalimu kuchonga madawati?

Hyo shule haina kamati ya Shule?
Mwalimu mkuu ni msimamizi wa miradi iliyopo shuleni kwake kwa kushirikiana na wataalamu kutoka halmashauri.

Manunuzi madogo kama hayo hayafiki hata 100M mwalimu mkuu anayasimamia. Mwalimu mkuu na mhusika mwingine hapo shule atatangaza tenda kwenye mfumo wa nest, na huu mfumo automatically utachagua mwenye gharama ndogo kati ya walioomba.

Ubora wa kazi unasimamiwa na engineer sasa mfano engineer alimuambia mwalimu kwamba hii kazi ipo sawa ni kumuonea mwalimu. Labda mbunge kajiridhisha kwamba kuna kona imechongwa hapo
 
Huyu naye mwehu tu tenda kapewa MZABUNI KWENYE MFUMO… mwalimu anahusikaje?
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Mwalimu mkuu ni msimamizi wa miradi iliyopo shuleni kwake kwa kushirikiana na wataalamu kutoka halmashauri.

Manunuzi madogo kama hayo hayafiki hata 100M mwalimu mkuu anayasimamia. Mwalimu mkuu na mhusika mwingine hapo shule atatangaza tenda kwenye mfumo wa nest, na huu mfumo automatically utachagua mwenye gharama ndogo kati ya walioomba.

Ubora wa kazi unasimamiwa na engineer sasa mfano engineer alimuambia mwalimu kwamba hii kazi ipo sawa ni kumuonea mwalimu. Labda mbunge kajiridhisha kwamba kuna kona imechongwa hapo
Unachongaje kona kwenye MFUMO ,hapo adili na mhandisi wa halmashauri aliyeyakubali na mzabuni SIO MWALIMU
 
Mimi siamini kama inashindikana kuchonga kona. Mfano labour inatakiwa kulipwa 18% - 25% ya gharama ya materials, kwamba ukilipa 25% hautakua umetoka nje ya matakwa.

Kwahiyo mtu anaweza kumlipa mzabuni wa labor 18% na 7% akabaki nayo
 
Sasa fundi si kawatengenezea madawati kulingana na pesa yao!! Elfu 70 unategemea dawati la ubora gani labda? Tena unatljitapa kabisa kama umetoa hela ya maaaaana.
 
Mbunge wa Tabora Mjini, Hawa Mwaifunga amekataa kupokea madawati 48 yaliyotengenezwa kwa ajili ya shule tatu katika jimbo hilo baada ya kuyakagua na kutoridhishwa na ubora wake, Septemba 18, 2026.

Madawati hayo yaligharimu kiasi cha Shilingi milioni tatu, fedha zilizotolewa kupitia Mfuko wa Jimbo, huku kila dawati likigharimu Shilingi 70,000.

Madawati hayo yaligawanywa kwa shule tatu, ambapo Shule ya Msingi Timkeni ilitengewa madawati 10, Shule ya Msingi Mihama madawati 10 na Shule ya Msingi Mpepo madawati 28.
Madawati hayo yalitengenezwa na Kampuni ya Diget, huku mchakato wa zabuni ukisimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Baada ya kukamilika, Mbunge Hawa Mwaifunga alifanya ukaguzi wa madawati hayo kabla ya kukabidhiwa kwa shule zilizokusudiwa. Hata hivyo, baada ya kuyakagua, hakuridhishwa na ubora wake na kuamua kutoyapokea.

Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo amedai kurejeshewa fedha zilizotumika katika utengenezaji wa madawati hayo, huku akitaka suala la ubora na mchakato wa utekelezaji wa mradi huo kufanyiwa ufafanuzi.

Tukio hilo sasa limeibua maswali kuhusu mchakato wa zabuni, matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo na udhibiti wa ubora wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za umma.
Alipigiwa kura na nani? aende huko sisi Tabora hatumtambui
 
Kwanini alitoa hela kabla?
 
Na yeye aache ujinga. Si angetengeneza mwenyewe mwenyewe hayo madawati!
 
Back
Top Bottom