Mbunge Hawa Mwaifunga akataa Madawati 48, asema “Mwalimu Nataka Milioni 3 Zangu”

Mbunge Hawa Mwaifunga akataa Madawati 48, asema “Mwalimu Nataka Milioni 3 Zangu”

Mbunge wa Tabora Mjini, Hawa Mwaifunga amekataa kupokea madawati 48 yaliyotengenezwa kwa ajili ya shule tatu katika jimbo hilo baada ya kuyakagua na kutoridhishwa na ubora wake, Septemba 18, 2026.

Madawati hayo yaligharimu kiasi cha Shilingi milioni tatu, fedha zilizotolewa kupitia Mfuko wa Jimbo, huku kila dawati likigharimu Shilingi 70,000.

Madawati hayo yaligawanywa kwa shule tatu, ambapo Shule ya Msingi Timkeni ilitengewa madawati 10, Shule ya Msingi Mihama madawati 10 na Shule ya Msingi Mpepo madawati 28.
Madawati hayo yalitengenezwa na Kampuni ya Diget, huku mchakato wa zabuni ukisimamiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Baada ya kukamilika, Mbunge Hawa Mwaifunga alifanya ukaguzi wa madawati hayo kabla ya kukabidhiwa kwa shule zilizokusudiwa. Hata hivyo, baada ya kuyakagua, hakuridhishwa na ubora wake na kuamua kutoyapokea.

Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo amedai kurejeshewa fedha zilizotumika katika utengenezaji wa madawati hayo, huku akitaka suala la ubora na mchakato wa utekelezaji wa mradi huo kufanyiwa ufafanuzi.

Tukio hilo sasa limeibua maswali kuhusu mchakato wa zabuni, matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo na udhibiti wa ubora wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za umma.
huyo hawa kaifanyia nini tabora mpaka leo😏
 
Wanawake bhna.....pesa yao ni ngumu sanaa ikitoka inatoka na maneno.

Mimi juzi nmechangia 1.5m kwa shule ya msingi uko kijijini kwa ajili ya hayo madawati kama mfanyabiara.....nmetumiwa picha tu kama shukran nikatulia.....sasa mbunge anawaka na camera juu
 
Wanawake bhna.....pesa yao ni ngumu sanaa ikitoka inatoka na maneno.

Mimi juzi nmechangia 1.5m kwa shule ya msingi uko kijijini kwa ajili ya hayo madawati kama mfanyabiara.....nmetumiwa picha tu kama shukran nikatulia.....sasa mbunge anawaka na camera juu.....
 
Back
Top Bottom