Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani, akichangia katika Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea jijini Dodoma leo Juni 18, 2025, amesema amekoshwa na majibu yaliyotolewa na Rais Samia kwa Mbunge Luhaga Mpina, akieleza kuwa yalimfurahisha na kumpa faraja.
"Nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwenye mkutano wake wa jana pale, amenikumbusha kwamba pale ambapo mwiba unaingilia ni pale pale mwiba unatakiwa utokee, kwahiyo bila kupoteza muda Mheshimiwa Rais alimjibu Mheshimiwa Mpina kwa vitendo kwamba anachokifanya hayuko sawa sawa.
Yale majibu ambayo alipewa Mpina mimi kwakweli yamenipa raha sana, yameniletea furaha sana. Mheshimiwa Rais kongole nyingi sana, hauwezi kuwa na mtoto umemzaa mwenyewe, ukamlea mwenyewe kwa tabu na raha halafu baadae anakuja kukupiga mateke hadharani, ulipoingilia mwiba, hapo hapo ndo unapotokea, Safi sana endelea kutuelekeza, endelea kutufundisha kwa vitendo mwisho wa siku tutaelewa tu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni nani."