Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Hawa ndio wabunge wetu tunaotarajia watupeleke mbele!amesema amekoshwa na majibu yaliyotolewa na Rais Samia kwa Mbunge Luhaga Mpina, akieleza kuwa yalimfurahisha na kumpa faraja.
Unatarajia nini kutoka kwa chawa? Anything boss anachosema ndio wanaelekea huko hukoMbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani, akichangia katika Mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoendelea jijini Dodoma leo Juni 18, 2025, amesema amekoshwa na majibu yaliyotolewa na Rais Samia kwa Mbunge Luhaga Mpina, akieleza kuwa yalimfurahisha na kumpa faraja.
"Nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwenye mkutano wake wa jana pale, amenikumbusha kwamba pale ambapo mwiba unaingilia ni pale pale mwiba unatakiwa utokee, kwahiyo bila kupoteza muda Mheshimiwa Rais alimjibu Mheshimiwa Mpina kwa vitendo kwamba anachokifanya hayuko sawa sawa.
Yale majibu ambayo alipewa Mpina mimi kwakweli yamenipa raha sana, yameniletea furaha sana. Mheshimiwa Rais kongole nyingi sana, hauwezi kuwa na mtoto umemzaa mwenyewe, ukamlea mwenyewe kwa tabu na raha halafu baadae anakuja kukupiga mateke hadharani, ulipoingilia mwiba, hapo hapo ndo unapotokea, Safi sana endelea kutuelekeza, endelea kutufundisha kwa vitendo mwisho wa siku tutaelewa tu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni nani."
viti maalum huyo,anategema huruma maalum. Hawezi kuwa na idependent thinkingKuna haja ya kubadili taratibu za kuwa mbunge.wabunge wengine ni mikosi tu
Inawezekana kweli alipata raha.Muimba taarabu na mcheza vigodoro wamekutana.
wananunua mitihaniNi daktari wa nini? Hii Nchi udaktari unachezewa sana
Uliowataja wote wanawindwa kuuwawa hawapo salamaMpina ni shujaa,Gwajima shujaa, Lissu shujaa, Warioba shujaa, na wachache wengine wenye ujasiri wa kumsahihisha dikteta bila hofu, wengi tu wanasubiria the right time wamu hit hard, jana nimeona Mh mpina akishangiliwa mno na wapiga kura wake alipokuwa akiwasemea mbele ya anayeitwa rais, ila rais mwenyewe alipoanza kutoa mipasho kwa mwakilishi huyo aliyepigiwa kura na wananchi hao niliona kabisa jinsi wananchi hao walivyosononeka, hakuna aliyeshangilia mipasho ya rais huyo, wengi walikuwa wameinamisha vichwa chini kwa masikitiko na kama vile kutoamini kile wanachokisikia kutoka kwa mtu waliyedhani kuwa ndiye tumaini lao, kwa kweli walisononeka sana, wakati wakirejea makwao karibu wote walikuwa wakihuzunika na kulalamika jinsi huyo mama alivyowakosea heshima kwa kumzodoa mwakilishi wao wanayemwamini na kumtuma akayaseme aliyoyasema kwa heshima kabisa, kwa kweli wananchi wale wamevunjika moyo sana, kama uliwatazama wakati wakimsikiliza rais ungeelewa ninachokisema.
Kati ya vitu dikteta Magu aliharibu ni kutuletea bunge la hovyoBunge hili limekusanya makahaba