Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. JANETH MAHAWANGA AWAHAMASISHA WANAWAKE KUFANYA KAZI KWA BIDII, UBUNIFU NA KUCHANGAMKIA FURSA
Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Janeth Elias Mahawanga kuwahamasisha Wanawake wenzangu kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, kuchangamkia fursa katika kilele cha kusherehekea Wiki ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2023.
Katika muendelezo wa Siku ya Wanawake Duniani akina mama wa Vicoba kutoka Taasisi Tano ambazo ni Buta Vicoba yenye jumla ya Vikundi 317, Jubi yenye vikundi 82, Omto yenye vikundi 57, Inuka yenye vikundi 30 na Sevia yenye vikundi 22 wameungana kusherehekea Siku hii kwa mafanikio makubwa.
Taasisi hizi tano zimeungana rasmi kufanya kazi pamoja kuhakikisha kila mwanamke anakuwa imara Kiuchumi lakini pia kuendelea kutoa ajira kwa vijana.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu wa 2023 inasema “Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia ni Chachu katika kuleta Usawa wa kijinsia” lakini manguli hawa wa Vicoba walikuwa na Kauli mbiu yao inayosema “Mwanamke na Uchumi Imara Inawezekana” na wameamua kuishi humo mwaka huu wote.
Vile vile, wamezindua “Vicoba Mfuko wa Ada” kwa ajili ya kuwekeza ada za watoto, wanataka ikifika mwezi January mwakani kila mmoja anaonyesha risiti za ada za watoto kama sehemu ya matunda ya ubunifu wa uwekezaji kupitia Vicoba kwani Vicoba ni uwekezaji na si umaskini.
Sambamba na hafla hizi akina mama hawa kila wanapokuwa na jambo lao lazima kuna fursa ndani yake ambapo zimetoka pikipiki kadhaa ambazo zitaenda ongeza ajira kwa vijana wetu sambamba na kutunisha mifuko ya vikundi.
"Niendelee kuwahamasisha Wanawake wenzangu kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, kuchangamkia fursa mbalimbali sambamba na kuitumia vyema Teknolojia kwani kwa hapa tulipofika hakuna namna ni lazima tuwe Wanawake wa Kidijitali kuendana na kiu yetu ya kutamani bidhaa ya Mwanamke Mjasiriamali wa Tanzania ivuke mipaka kwenye Mataifa mengine." - Mhe. Mahawanga
#TishaMama
#MamaVicoba
#ItazameDarKiutofauti
#Kaziiendelee