Pre GE2025 Mbunge Jerry Silaa akataliwa na Wananchi wa Jimbo la Ukonga mbele ya Waziri Ulega

Pre GE2025 Mbunge Jerry Silaa akataliwa na Wananchi wa Jimbo la Ukonga mbele ya Waziri Ulega

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kazi ya usimamizi hufanywa na mkuu wa wilaya akishirikiana na wakurugenzi ambaye anasaidiana na engineer wa wilaya. Ndiyo maana hujawahi kusikia mbunge anatumbuliwa kwasabb mradi fulani haujakamilika ama kuna ufisadi. Wanaotumbuliwa ni wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wahandisi.
Unamtumbua vipi mtu ambaye kachaguliwa na wananchi!

Sioni umuhimu wa mbunge mpaka sasa kwa maelezo yako, kama yeye anapaswa kuwa msemaji katika Jimbo lake. Na sielewi hiko cheo ni cha nini.
 
Amna anachofanya huyo, ukonga barabara mbovu, hio rami y kuanzia mombasa kwenda moshibaha imejengwa chini ya kiwango.

Kipande cha moshibaha kwenda kwa diwani barabara ni mbovu hakuna mfano.
Ardhi zao zina maji na soil profile mbovu sana, ipo haja kwa huko tuendako tukatumia zaidi concrete roads, itaokoa hata gharama za kuziba viraka kila wakati.
 
Jerry hakuna anachokifanya, barabara nyingi ukonga ni mbovu hasa kipindi hiki cha mvua. Ni mmoja wa wabunge watakaopata shida uchaguzi ujao.

Pamoja na kwamba Mimi sio mwana Ukonga ila Kwa uzoefu wangu Tanzania hasa mjini watu Huwa hawachagui Mbunge Kwa kuangalia kama ametekeleza Ilani kwa Asilimia ngapi.

Mfano huko Ukonga wamekuwa na Wabunge dizaini ya Mwita Waitara Kuna Cha maana walipata?

Ni mara mia Jerry Silaa kuliko hao waliopita.Kama ni Barabara Mbona Jerry kajitahidi?

Mwisho ni Majimbo ya Vijijini tuu ndiko Wananchi humchagua Mbunge Kwa Kwa masuala waliyokubaliana huko Mjini ni ujinga na uzushi wowote ambao watu wataona kwao inafaa.

Harafu hatutegemei watu wote wakukubali, haiwezekani.
 
Jerry hakuna anachokifanya, barabara nyingi ukonga ni mbovu hasa kipindi hiki cha mvua. Ni mmoja wa wabunge watakaopata shida uchaguzi ujao.
Hata mnyika alikuwa mbunge wa kibamba zaidi ya muongo mmoja na hakuna alichofanya mbaka Leo kibamba Ina shida ya maji na barabara baada ya kujua atapigwa chini na wananchi akaamua ajifiche kwenye kivili Cha ukatibu mkuu
 
Hakuna Mbunge wa Ovyo kupita Slaa. Kutoka Banana kwenda Kitunda ile Barabara ni fedheha kuwa karibu na Airport.
Mvua zote zilizonyesha na watu kulalamika hata mara moja hajapeleka maskio yake marefu kufanya tathmini tu.

Slaa labda akatoe kafara ya mtu ndio ataweza kurudi tena Bungeni.
 
Ukonga kuna barabara mbovu na maji ya shida. Hata Segerea maji tatizo. Wananchi wa majimbo hayo mawili hawaogi na ni wachafu hasa kwenye daladala, tena ukutane na wanawake wa Kitunda weusi tii, wamepiga mkorogo alafu wana mawigi yanatema.
Mtu anakazana kupita kwenye vumbi akifika kwake maji ya kuoga hamna.

Atakayesema nimetukana basi aende Banana ajionee vipanya vya kwenda Kitunda uko.
Sasa hili dongo ni la Slaa au wakazi wa Kitunda😂😂😂?
 
Kazi ya mbunge ni uwakilishi . Anachukua maoni, shida, mipango na matamanio ya wananchi wa jimboni
Hapo sasa ndipo anapofeli Bw. Slaa. Hawakilishi jimbo, hachukui maoni, shida wala matamanio ya wananchi wake.

Moja ya matamanio ya wakazi wa Ukonga ni barabara ambazo hazitamaniki.

Kwahiyo kwa njia moja ama nyingine amefeli kuwezesha upatikanaji wa barabara kwa kushindwa kufikisha maoni ya anaowakilisha.
 
Back
Top Bottom