Pre GE2025 Mbunge Jerry Silaa akataliwa na Wananchi wa Jimbo la Ukonga mbele ya Waziri Ulega

Pre GE2025 Mbunge Jerry Silaa akataliwa na Wananchi wa Jimbo la Ukonga mbele ya Waziri Ulega

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa hili dongo ni la Slaa au wakazi wa Kitunda😂😂😂?
Wote kwa pamoja. Wananchi waache kuchagua viongozi wapuuzi wenye mabegi ya vyeti ila utendaji sifuri mwishowe wanaishia kushindwa majukumu madogo kabisa hivyo kuathiri maisha ya kila siku ya mwananchi.

Viongozi waache kutumia akili zao za kuokotoea vyeti vingi kujifanya wanaongea vitu vikubwa wakati vitu vidogo kabisa hawawezi. Elimu ya Slaa haina msaada wowote kwa jimbo wala kwa taifa, kila tamko lake limejaa ujinga utadhani ni illiterate.
 
Hakuna Mbunge wa Ovyo kupita Slaa. Kutoka Banana kwenda Kitunda ile Barabara ni fedheha kuwa karibu na Airport.
Mvua zote zilizonyesha na watu kulalamika hata mara moja hajapeleka maskio yake marefu kufanya tathmini tu.

Slaa labda akatoe kafara ya mtu ndio ataweza kurudi tena Bungeni.
Wale wauza mayai wa Dar wengi wanatokea Mkoa wa Mara, hasa Tarime, lazima watatumia akili za Tarime.

Ndio maana anahangaika kutafuta hela kutoka kwa wemye vituo vya mafuta ili "kurahisisha" uchaguzi
 
Kwa mbeleko ya kizimkazi atapita tena kwa kishindo na hasa ikizingatiwa kuwa aliutetea sana mkataba wa kugawa mali bure kwa wajomba
Jerry slaa akipata hata kura 100 kwa wanachi wa ukonga sijui.
Hakuna anayempenda labda wampitishe kwa mabavu.

Wananchi wa ukonga ndio tunajua ukweli atapita kwa mabavu si kwa kura za wananchi.

Pale mombasa ramani ilitakiwa ianzie kambi ya FFU zamani ilipobomolewa inyooshe kupitia relini moja kwa moja mpaka mto msimbazi, hakuna lililofanyika.

Daraja lililojengwa ni la ulongoni A, daraja la msimbazi liliondoka na maji wakaja wahuni wakabeba nondo na matofali, hakuna daraja lililopigwa pesa kama lile lilikuwa kituko mchanga mtupu.

Ile njia ilipaswa kutoka kwenda mpaka daraja la njia panda segerea la chuma, na kwenda kukutana mombasa.

JERRY SLAA HAKUNA ATAKAYEMCHAGUA LABDA WAENDELEE KUIBA KAMA WALIVYOZOEA
 
Huwa pesa za bajeti zikitoka kwa ajili ya Jimbo Fulani mbunge anafahamu na anasimamia au anakuwa yupo pembeni kabisa na hausishwi?

Nipo kujifunza
Sio kazi ya mbunge kusimamia miradi ya maendeleo. Utekelezaji unafanywa na halmashauri (au serikali kuu), na vyombo vyombo hivyo ndio vinatakiwa kuwajibika kikamilifu. Mfano, barabara au jengo likijengwa chini ya kiwango ktk hatua mbalimbali za utekelezaji, mbunge hawezi kujua sababu sio taaluma yake, wala sio jukumu lake. Wataalam wako halmashauri na serkalini.
 
Serikali mkuu; mawaziri, maRC, maDC na wakurugenzi.
Kwanini kazi ya mbunge kwenda kusema tu matatizo bingeni?

Wana kazi gani hawa watu?
Mkuu mbunge wanachaguliwa kwenda bungeni;

1. Kuwakilisha maoni na kero za wanajimbo bungeni.

2. Kutunga sheria bungeni.

3. Kuisimamia serikali bungeni.
Ufafanuzi namba 2, Sheria wanazotunga ni za bunge? Au za wapi?
 
Jerry slaa akipata hata kura 100 kwa wanachi wa ukonga sijui.
Hakuna anayempenda labda wampitishe kwa mabavu.

Wananchi wa ukonga ndio tunajua ukweli atapita kwa mabavu si kwa kura za wananchi.

Pale mombasa ramani ilitakiwa ianzie kambi ya FFU zamani ilipobomolewa inyooshe kupitia relini moja kwa moja mpaka mto msimbazi, hakuna lililofanyika.

Daraja lililojengwa ni la ulongoni A, daraja la msimbazi liliondoka na maji wakaja wahuni wakabeba nondo na matofali, hakuna daraja lililopigwa pesa kama lile lilikuwa kituko mchanga mtupu.

Ile njia ilipaswa kutoka kwenda mpaka daraja la njia panda segerea la chuma, na kwenda kukutana mombasa.

JERRY SLAA HAKUNA ATAKAYEMCHAGUA LABDA WAENDELEE KUIBA KAMA WALIVYOZOEA
Na ndiyo maana Jerry anajikomba kwa kizimkazi maana anajua nyie wananchi hamtaki🤣😆
 
Back
Top Bottom