Nakuji
Ngoja nikujibu kwa mara ya mwisho. Kukataa kuwa uhuru wa kujieleza na kukosoa ni nguzo mojawapo ya maendeleo inaonyesha fikra zako zilivyo duni. Hivi unadhani bila uhuru wa kukosoa na kujieleza wananchi wanawezaje kuifahamisha serikali kuhusu utendaji mbovu wa wale waliopewa dhamana ya kuwasaidia ili wapate maendeleo? Tumeona utilities wa miradi ya maji isiyotoa maji, barabara zinazoharibika baada ya msimu mmoja ambapo wananchi inabidi wamsubiri Rais ndio watoe dukuduku zao. Uhuru ungekuwepo, matatizo yangemalizika katika ngazi ya DED. Tumeona madaktari wakiogopa kutoa takwimu kuhusu ugonjwa wa Covid kwa kuogopa kushughulikiwa.
United Airlines ni mali ya United Airlines Holdings Inc, kampuni ya kibiashara. Swiss Air ilifilisika na ikafutwa kabisa. Swiss International Airlines imetokana na Cross Air. Ni Crossfire ndio iliyobadilisha jina kuwa Swiss International Airlines. Hayo unayosema kuhusu unayoita mashirika mkakati ni upuuzi tu na zinatokana na kuangalia mno Netflix. Tunashauriwa tusiwe na shirika la ndege la serikali simply kwa sababu hatuna uwezo wa kulihudumia na kuliendesha ipasavyo. Tunajenga hoja kuwa tunanunua ndege ili tulete watalii halafu tunaogopa kwenda huko kwenye watalii kwa kuogopa kuwa zitakamwatwa. Kama tuna mihela mengi kiasi hicho kwa nini tusiwalipe tu wanaotudai? Au kwa nini tusifanye kama walivyofanya waswiss ( Na CAG wa zamani alivyoshauri) kwa kuiacha ATCL ifilisiwe na madeni yafe nayo. Baada ya hapo ndio tujipange kuanzisha shirika lingingine kama tutaona kuna haja ya kufanya hivyo. Nje ya hivyo tutaishia kupeleka Dreamliner Mwanza na Zanzibar.
Regulators kazi yao ni kuhakikisha kuwa umeme wa kutosha unapatikana na kwa bei inayoeleweka. Mambo ya uende wapi au usiende wapi ni mambo ya kibiashara na soko litaamua. Hayo Mambo ya serikali kutaka kuamua umeme ukatwe wapi na ukatwe lini ndio umechangia sana uharibikaji wa mitambo yetu. Hayo maamuzi yanapaswa kufanywa na wataalamu na sio wanasiasa.
Of course, energy distributors wanafanya kazi kwa maslahi ya serikali zao kwa kulipa kodi na kufuata matakwa ya kisera ( sio uendeshaji wa serikali). Kama malengo ya serikali ni kuondokana na fossil fuels nao watawekeza kwenye nishati safi zaidi maana serikali itawaadhibu kwa kuendelea kutoa nishati chafu. Kama hata hilo haulielewi basi hautakuja kuelewa kitu hata kama tukishinda humu siku nzima. Kwa sababu hiyo, sitakujibu tena maana itakuwa kujipotezea muda.
Amandla...
Nakujibu mara ya mwisho pia. Mwisho tukubaliane kutokukubaliana.
Nimekupinga kwenye suala la uhuru wa kujieleza na kukosoa ulivyoliweka kwa uzito sawa na huduma bora za afya na maji safi na salama, lakini namna ulivyolijibia nimeona wazi wazi kabisa kwamba haupo consistent kabisa katika kufikiri kwako kuhusu dhana ya "uhuru wa kujieleza na kukosoa". Lakini hainishangazi sana maana mengi ya mawazo ya watu wa aina yenu siyo original ideas, mnaparrot tu vimisemo mnavyolishwa tu na systems za huko, bila hata kujua nini na kwa nini.
"Tumeona utilities wa miradi ya maji isiyotoa maji, barabara zinazoharibika baada ya msimu mmoja ambapo wananchi inabidi wamsubiri Rais ndio watoe dukuduku zao. Uhuru ungekuwepo, matatizo yangemalizika katika ngazi ya DED."
So wananchi walimsubiri Rais wakatoa dukuduku zao. Kumbe uhuru wa wananchi wa kujieleza na kukosoa upo, kiasi kwamba waliweza kuuonyesha hata mbele ya Rais. Argument yako ni nini hasa? Uhuru wananchi wanao hawana? Kama walisubiri hadi Rais aje ndio wauonyeshe walishindwa vipi kuuonyesha kwa viongozi wa ngazi za chini? Sioni kama hili ni tatizo la uhuru wa kujieleza na kukosoa, naliona kama tatizo la elimu ya uraia kwa ujumla, wananchi hatujui nini cha kufanya tunapoona watendaji wa serikali wanafanya vibaya.
"Tumeona madaktari wakiogopa kutoa takwimu kuhusu ugonjwa wa Covid kwa kuogopa kushughulikiwa."
Sikuelewi yaani. Takwimu zilikuwa zinatolewa, baada ya kushauriana wenyewe kwa wenyewe huko serikalini kwamba takwimu zinazidisha hofu ya Covid-19 kwa wananchi na kuwapanikisha watu wakatoa agizo zisitolewe. Hata upimaji wa Covid-19 ukasitishwa. Bila shaka takwimu halisi za Covid-19 hazikuwepo pia. Unahesabu hili kama kuminywa kwa haki za "uhuru wa kujieleza na kukosoa" wa madaktari? Kama unalihesabu hilo kwenye uhuru wa aina hiyo basi you are totally irredeemable. Hili si suala uhuru wa kujieleza na kukosoa, hili ni suala jingine kabisa -- liite suala la nchi kufanya tofauti na jumuiya ya kimataifa kwenye inshu ya Covid-19. Kuna watu walikosoa msimamo huo wa serikali, na kuna watu walikubaliana na msimamo huo wa serikali. Nilitegemea watu kama nyie wenye uelewa basic (aina ya uandishi wako unaniaminisha hivyo) mngeweza kuwa objective katika kufanyia analysis mambo kiasi kwamba inapokuja suala la kukosoa serikali pale mnapofanya hivyo hata serikali inakubali kwamba kweli hapa tulipotoka, ngoja tujirekebishe. Lakini mnavyokosoa kosoa kila kitu, serikali hupata shaka kama mnafanya hivyo kwa nia njema au mna ajenda.
Kwenye mambo ya airlines (SwissAir, n.k), na kwenye mambo ya umeme (regulation, n.k), na namna gani mashirika ya aina hii ni vital kwenye Geo-Economic-Security interests za nchi, naona nisiendelee tena kujibishana. Endelea na msimamo wako na mimi nitaendelea na wa kwangu.