Ninajitahidi sana nikujibu kistaarabu, lakini unanipa tabu sana. Lakini ngoja niendelee hivyo hivyo.
Umeandika mengi lakini nilipofika ulipoandika "uhuru wa kujieleza na kuikosoa serikali yao" ukanichefua. Yaani katika vipimo vya maendeleo kubwabwaja kinyume na taifa lako nayo unaita kipimo cha maendeleo? Na nieleweke, kwamba sitaki kusema unyimwe uhuru wa kujieleza au kukosoa.... lakini nimeshangaa sana namna gani nyie watu mnameza kila kitu mnacholishwa na systems za kibeberu kiasi cha kuweka uhuru wa kukosoa kwenye mizania sawa na huduma bora za afya.
"Nchi nyingi tu hazina mashirika yake ya ndege ( Marekani, Uswisn.k.) na yanaenda vizuri tu."
Soma United Airlines na Swiss International Airlines (zamani SwissAir). Nimekwambia nchi zote duniani zinazojielewa zipo inshu fulani hivi za kinchi ambazo hufanyika kwa wepesi zaidi au kwa maslahi mapana ya nchi yako iwapo una shirika la ndege imara ambalo serikali inaweza kulitumia kwa muktadha huo. Hakuna serikali functional isiyo na shirika lake la "kimkakati" kwa maslahi ya nchi husika. Ukiona mtu au kikundi cha watu kinatushauri tusiwe na shirika la ndege la serikali ujue huyo mtu au hicho kikundi kina ajenda zake. Nchi kama Marekani zipo sophisticated zaidi; na kutokana na nguvu za kiuchumi walizo nazo wana uwezo hata wa kuficha interests za kinchi kwenye private sector, au kujidisguise ionekane kama ni corporate private entity lakini kumbe inaserve interests za nchi ya Marekani.
"Tangu lini Tanesco na ATCL zimekuwa mashirika ya kimkakati"
"Nchi karibu zote za ulaya usambazaji wa nishati unafanywa na mashirika binafsi. Kazi ya serikali ni ku regulate tu."
Huelewi hata ninaposema kimkakati ninamaanisha nini. Unaposema kazi za serikali nchi za Ulaya ni "kuregulate tu" hata hujaeleza nini kilichomo kwenye kuregulate, wanaregulate nini, serikali imeingia mikataba ipi nao hao private generators and distributers? Hata sisi hapa TANESCO ina (ishawahi) kuwa na mikataba na private generators, refer Songas, IPTL, n.k. La muhimu ni to what extent serikali ina control energy sector. Kama level ya regulation haiziruhusu serikali za nchi hizo kuamua umeme uende wapi, ukatwe wapi, usiende wapi na kwa nini, then nchi hizo zitakuwa miongoni mwa nchi dhaifu sana kiusalama. Hata hivyo hii ni kukufumbua macho tu kwamba usidanganywe na neno "regulation". Hao energy suppliers na distributers wa Europe ni insiders wa European governments, wanaoperate kwa niaba ya serikali zao, kwa maslahi ya serikali zao. Nchini mwetu tulijaribu kuexperiment hiyo model na IPTL kilichotokea tukawa tunapigwa 120M kila siku mitambo iwe on au off.