Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE MHE. JULIANA DANIEL SHONZA - "MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN IMEKUWA CHACHU YA MAFANIKIO KWA TAIFA
Mbunge wa Viti Maalum CCM Wanawake (UWT) anayetokea Mkoa wa Songwe Mhe. Juliana Daniel Shonza amempongeza Rais Samia kwa kutimiza Miaka Miwili Madarakani huku akijikita kwa kuelezea miradi mbalimbali ya kimaendeleo iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa na Serikali kwa kipindi cha Miaka Miwili ya Rais Samia katika Mkoa wa Songwe.
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NA UJENZI WA MIRADI MIPYA YA MAENDELEO MKOA WA SONGWE
Ndani ya Miaka Miwili, Mkoa wa Songwe ulizingatia vipaumbele vifuatavyo;
1. Kutatua migoggoro ya ardhi
2. Kudhibiti mauaji ya wananchi,
3. Kudhibiti uharibifu wa mazingira,
4. Kutatua kero za wananchi kwa wakati
5. Kuimarisha Diplomasia ya Uchumi
6. Kukuza uhuru wa kufanya biashara
Katika ya Machi 2021 - Machi 2023 chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungango wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Songwe ulipokea fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kwa mchanganuo ufuatao;
1. Sekta ya Elimu - Tsh. 67,519,816,682.47
2. Sekta ya Afya - Tsh. 39,960,109,728.39
3. Sekta ya Maji - Tsh. Sh. 30,705,241,410.39
4. Sekta ya Barabara - Tsh. 193,000,000 (TANROADS - Tsh. Sh. 129,055,760,000; TARURA - TSh. 8,168,385,625.56; PRNG - TSh. 1,600,000,000)
5. Sekta ya Kilimo - Tsh. 25,594,643,867
6. Sekta ya Ardhi - Tsh. 2,093,319,000
7. Sekta ya Utawala - Tsh. 7,271,458,000
8. Sekta ya Nishati - Tsh. 4,958.887,513.83
✅ SEKTA YA ELIMU
Kuanzia mwezi Machi, 2021 hadi Februari, 2023 Sekta ya Elimu Mkoa wa Songwe imepokea jumla ya shilingi 67,519,816,682.47 na kutekeleza miradi ifuatayo;
1. MRADI WA EP4R - Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari kupitia programu ya EP4R (Madarasa 57, Matundu 181 ya Vyoo, Nyumba 3 Tunduma, Mabweni 2 Tunduma na Momba)
2. Maabara Shule za Sekondari - Maabara 33 zimejengwa. Wilaya ya Mbozi maabara 13, Wilaya ya Songwe Maabara 7, Halmashauri ya Tunduma Maabara 6, na Wilaya ya Ileje maabara 7.
3. Ukamilishaji wa Maboma ya Madarasa 37 ambapo Wilaya ya Mbozi Maboma 18, Wilaya ya Songwe Maboma 9, na Wilaya ya Ileje Maboma 10
✅ SEKTA YA AFYA
Katika kipindi cha Miaka Miwili tangu kuanza kwa utawala wa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Machi 2021, katika Sekta ya Afya Mkoa wa Songwe umepokea Shilingi 39,960,109,728.86/=
1. Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe
2. Ujenzi wa Hospitali nne za Wilaya ya Momba, Tunduma, Songwe na Ileje
3. Ujenzi wa vituo vya Afya 6 vya Tarafa kwa fedha za tozo (Tunduma 1, Songwe 1, Ileje 1, Momba 1 na Mbozi 2)
4. Ujenzi wa vituo vya Afya 7 kwa Ruzuku ya Serikali (Tunduma 3, Songwe 1, Ileje 1, Momba 1 na Mbozi 1)
5. Ukamilishaji wa Maboma 39 ya Zahanati (Tunduma 4, Songwe 8, Ileje 8, Momba 9 na Mbozi 10)
6. Mpango wa Maendeleo ya Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 (IMF)
7. Usafi wa Mazingira (WASH) Vyoo 68 (Songwe 14, Ileje 6, Momba 24 na Mbozi 24).
8. Fedha za Mfuko wa Pamoja wa Afya (HSBF)
9. Fedha za udhubiti wa UKIMWI-Walter Reed
10. Ulinzi wa Mtoto kupitia programu ya UNICEF
✅ SEKTA YA MAJI
RUWASA Mkoa wa Songwe kati ya Machi, 2021-Machi, 2023 ilipokea fedha kutoka P4R, COVID-19 na Mfuko wa Maji (NWF) Jumla ya kiasi cha Shilingi 30.705,241,410.39 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maji vijijini kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Songwe wanapata huduma ya Maji kutoka 73.3% hadi 85% ifikapo Juni 2023 kwenye Miji na Vijijini kwa kuzingatia malengo ya uanzishwaji wa RUWASA.
✅ SEKTA YA BARABARA
1. Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)
Mkoa wa Songwe kupitia Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) umetekeleza miradi 11 yenye thamani ya Shilingi 129,055,760,000.
- Barabara Kuu ya Mpemba Isongole km 50.3
- Barabara ya Mkoa ya Katumba Songwe–Kasumulu–Ngana–Ileje km 123
- Barabara ya Mkoa ya barabara ya Ruanda–Nyimbili–Hasamba–Izyila–Itumba km 79.7
- Barabara ya Mkoa ya barabara ya Chang’ombe–Mkwajuni–Patamela–Makongolosi km 111.6
- Barabara Kuu ya Tanzam, Sogea–Tunduma
- Barabara ya Mkoa ya Chang’ombe–Mkwajuni–Patamela
- Daraja la Nakambekezwa barabara ya Mkoa ya Shigamba–Itumba–Isongole
- Daraja la Songwe barabara ya Mkoa ya Galula–Namkukwe
2. Wakala wa Barabara Mijini & Vijijini (TARURA)
Mkoa wa Songwe kupitia Wakala wa barabara Mijini & Vijijini (TARURA) umetekeleza miradi 3 yenye thamani ya Shilingi 16,174,292,602.
- Barabara za Lami zimeongezeka kutoka km 15.74 - km 19.54
- Barabara za Changarawe zimeongezeka kutoka km 727.92 - km 760.49
- Barabara za Udongo zimepungua kutoka km 2,597.97 - km 2,561.60
✅ SEKTA YA NISHATI
1. Kupitia mradi wa REA AWAMU YA TATU MZUNGUKO WA PILI Mkoa wa Songwe umepokea Shilingi 42,383,195,639.68, Kati ya Vijiji 307 vya Mkoa wa Songwe idadi ya Vijiji vyenye umeme imeongezeka kutoka Vijiji 180 hadi Vijiji 219.
2. Urefu wa njia ya Umeme wa Msongo wa Kati (MV line) 33kV umeongezeka kutoka
1244.79 km-1326.26 km
3. Urefu wa njia ya Umeme wa Msongo Mdogo (LV line) 0.4kV umeongezeka kutoka
867.03km-1006.37km
4. Idadi ya Transfoma za kupoza Umeme kwa ajili ya matumizi ya wateja zimeongeka
kutoka idadi ya 595-730
5. Idadi ya Wateja waliounganishwa Umeme imefikia 83,224 kutoka 56,027
6. Shilingi 2,473,637,171.92/= ilitolewa kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya kupeleka Umeme. Jumla ya miradi 66 ilitekelezwa; Miradi 17 ilipeleka umeme kwenye Taasisi za Kiserikali; Miradi 20 ilipeleka umeme kwa wawekezaji mbalimbali na Miradi 29 ilipeleka umeme kwa wananchi.
✅ SEKTA YA KILIMO
Mkoa wa Songwe umepokea Shilingi 25,594,643,867 kwa ajili ya uendelezaji wa Sekta ya Kilimo na Mifugo
- Uendelezaji wa Kilimo cha Korosho
- Uendelezaji wa Kilimo cha Kahawa
- Uendelezaji wa Kilimo cha Michikichi
- Ununuzi wa Mahindi ya wananchi kupitia NFRA
- Mikopo kwa vyama vya ushirika
- Uwezeshaji wa vitendea kazi (Pikipiki) kwa maafisa ugani
- Uendelezaji wa Sekta ya Mifugo kupitia ujenzi wa Majosho
- Dawa za kuogeshea Mifugo
✅ SEKTA YA MADINI
Machi, 2021 hadi Feburuari 2022, Uzalishaji wa Madini kwa wachimbaji wadogo kupitia soko la Madini la Songwe ni kilogramu 1,040 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 121, Uchimbaji Mdogo wa Madini ya Dhahabu umechangia Jumla ya Maduhuli Shilingi Bilioni 8.83 (Mrabaha ni Shilingi Bilioni 7.26, Ada ya Ukaguzi Shilingi Bilioni 1.21 na Ushuru wa Huduma kwa Halimashauri Shilingi Milioni 363.1). Ofisi imefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 25.69.
✅ SEKTA YA UTAWALA
Mkoa wa Songwe, jumla Shilingi 281,128,987,495.00 zimetumika kushughulikia maslahi ya watumishi kuhusiana na Upandaji wa Madaraja, Ulipaji wa Mapunjo ya Mishahara, Ajira mpya, Ulipaji wa Madeni, Kulipa posho ya Madaraka kwa Maafisa Watendaji wa Kata 94 na posho za Madiwani 126 wa Halmashauri. Jumla ya Watumishi 2,220 walipandishwa vyeo na Watumishi 694 waliajiriwa.Serikali kuwezesha Miundombinu ya kufanyia Biashara
Machi, 2021 - Machi, 2023, Serikali ya Awamu ya Sita imewezesha ujenzi wa Miundombinu ya kufanyia biashara katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma kwa kutoa jumla ya Shilingi 383 Milioni kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo (wamachinga). Mkoa wa Songwe umepokea kiasi cha Shilingi 10 Milioni kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Machinga Mkoa eneo la Nselewa karibu na Ofisi za Mkuu wa Mkoa.
MIKAKATI YA MKOA WA SONGWE
1. Kujenga Bandari Kavu, Mpemba Halmashauri ya Mji wa Tunduma2. Kufufua na kupanua shughuli za machimbo ya Makaa ya Mawe mgodi wa Kiwira, Ileje na kufunga mtambo wa kuzalisha mkaa mbadala kwa matumizi ya nyumbani kwa kutumia makaa ya mawe.
3. Kuendelea kushirikiana na Wizara ya Madini kuhakikisha mwekezaji wa mgodi wa Madini Adimu anapata leseni ya kuanza uchimabaji wa Madini ili kusisimua Uchumi wa Mkoa wa Songwe.
4. Kuendeleza jitihada za utunzaji wa Mazingira kwa kupanda Miti, kurudisha Uoto wa Mto Zira ili kuepusha athari za mabadiliko ya tabianchi.
5. Kuimarisha mfumo wa Masoko kwa njia ya ushirika na kusimamia kilimo cha mkataba na kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima.
Attachments
-
WhatsApp Image 2023-03-23 at 12.20.58.jpeg60 KB · Views: 10 -
WhatsApp Image 2023-03-23 at 11.14.32(4).jpeg68.7 KB · Views: 11 -
WhatsApp Image 2023-03-23 at 12.02.53.jpeg56 KB · Views: 11 -
WhatsApp Image 2023-03-23 at 11.14.32(1).jpeg112.4 KB · Views: 9 -
WhatsApp Image 2023-03-19 at 12.28.16.jpeg92.4 KB · Views: 10