Mbunge Kikoyo: Sheria ya Bima ina matatizo makubwa, hatuwatendei haki wananchi

Mbunge Kikoyo: Sheria ya Bima ina matatizo makubwa, hatuwatendei haki wananchi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Dkt. Oscar Kikoyo Ishengoma amesema Sheria ya Bima hususan kwenye makosa yanayotokana na ajali za barabarani ina matatizo makubwa.

Amesema, "Ukisoma hii Sheria, ajali inapotokea barabarani Jeshi la Polisi watapima, Kesi itapelekwa Mahakamani Hukumu itoke kisha Mhanga aiambitishe ili kwenda kudai fidia"

Ameeleza, "Tatizo kubwa ni Mhanga wa ajali anapokwenda kudai ile fidia, Sheria ya Bima ipo kimya. Kiasi anachoenda kulipwa ni maamuzi ya Kampuni ya Bima. Hatuwatendei Haki watu wetu"
 
Bima ya Tanzania ni wizi mtupu! Kwa kifupi ni njia ya serikali kupata mapato bila jasho ndiyo sababu watu huishia kukata third party insurance kwa sababu bima ni takwa la kisheria.
 
kama mhanga hana pesa ya matibabu anasubiria maamuzi ya kesi kaburini
 
Bima ya Tanzania ni wizi mtupu! Kwa kifupi ni njia ya serikali kupata mapato bila jasho ndiyo sababu watu huishia kukata third party insurance kwa sababu bima ni takwa la kisheria.
Ndio maana wanalazimisha.
Wafanye option...halafu makampuni mbalimbali yaingilie kushawishi jamii kama kwa mitandao ya simu uone kama watu hawatakiwi wengi
 
Bima ni wezi kama jeshi la zimamoto na vile vi fire extinguisher vyao uchwara, unalipia lakini siku ukipata shida wanakushangaa, kiukweli kuna baadhi ya huduma za serikali zinaakisi kuwa serikali ni mwizi kama wezi wengine
 
Anaekata comprehensive na third party msoto ni ule ule..yaan had ulipwe inavyotakiwa. .utahenya sanaaa..yaan bima watoe chao kirahis...hiawezekn
 
Unweza kutuambia umeelewa nini?ana maana gani?

Mfano: mkipata ajali kwenye basi ukaumia labda umevunjika mguu,

No 1: Itabidi ujitibu kwa gharama zako huku ukisubiri kesi iishe mahakamani.

Je, kama huna hela itakuwaje? Hapa anazungumza kwamba kunatakiwa sheria ipaangalie vizuri.

No 2: Kesi ikiisha ukaenda kudai kwenye Bima, wao wataamua wakulipe kiasi gani.

Hapa ndipo pia anapazungumzia, kwamba kuwe na sheria inayowabana kutomlalia muhanga.

Hivyo ndivyo nilivyo elewa.
 
OK nashukuru kwa maelezo
 
Back
Top Bottom