Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu amempongeza mwanamuziki Godfrey Tumaini maarufu Dudu Baya kwa juhudi zake za kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda maadili, akimtaja kuwa ni mpambanaji wa maadili na “Balozi wa Wabunge” katika kampeni yake ya 'Linda Mgongo wako'.
Kingu amesema ujumbe wa “Watch Your Back”, unaomaanisha “Linda Mgongo”, una umuhimu mkubwa katika jamii kwa kuwa unahamasisha watu kuwa makini katika kulinda maadili na mustakabali wa kizazi kijacho.
Amesema suala la malezi na maadili linapaswa kuanzia katika familia, akieleza kuwa kila asubuhi watoto wake wanapojiandaa kwenda shule, huwapa wosia na kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia ujumbe huo wa “Linda Mgongo”.
Vilevile Mbunge huyo wa Singida Magharibi amesema, kampeni hiyo ina umuhimu katika kuwajenga vijana kuwa na uelewa kuhusu maadili na kuwasaidia kuepuka mienendo inayoweza kuathiri maisha yao na jamii kwa ujumla.
Katika kuunga mkono juhudi hizo, Kingu amesema yeye pamoja na rafiki yake wameamua kuchangia jumla ya Shilingi milioni 1.5 (TSh 1,500,000) kwa ajili ya kuendeleza kampeni hiyo ya kuhamasisha na kulinda maadili ya vijana.
Katika hatua nyingine, Kingu ametoa wito kwa jamii kushirikiana katika juhudi za malezi na ujenzi wa maadili, akisisitiza kuwa jukumu la kulinda kizazi kijacho linahitaji ushirikiano kutoka kwa wazazi, viongozi na jamii kwa ujumla.