Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Mbunge wa Nyasa Mkoani Ruvuma, John Nchimbi ameitaka Serikali kuwapanga watumishi wake kulingana na weledi wao, ili kuepusha kuwapanga maeneo yasiyowahusu na hivyo kuzorotesha ufanisi katika kazi.
Nchimbi aliyasema hayo April 17 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia hotuba ya mapato na Matumizi ya Wizara Nchi katika Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), akiitaka wizara hiyo pia kuwa na Bodi ya Mishahara itakayokuwa inasimamia mishahara ya watumishi ili
Nchimbi pia ameitaka Serikali kusimamia Mwongozo wa kuwapatia motisha watumishi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu, akisema licha ya mwongozo huo kupitishwa mwaka 2010, haujawahi kutumika mpaka leo.
Pia Nchimbi amekosoa utaratibu wa Utumishi kujittwisha jukumu la kuajiri watumishi wote nchini, tofauti na zamani, ambapo mashirika na taariri za umma zilikuwa na utaratibu wake wa kuajiri.