Mbunge: Kwanini mwananchi akileta TV Bara kutoka Zanzibar analipia kodi wakati nchi ni moja?

Mbunge: Kwanini mwananchi akileta TV Bara kutoka Zanzibar analipia kodi wakati nchi ni moja?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Haiwezekani mwananchi amesafiri kutoka Zanzibar na TV moja used anakuja kutumia nyumbani anafika Bara anaambiwa alipe kodi na hii ni nchi moja, akini anayetoka Morogoro kwenda Dar halipi kodi, lakini anayetoka Zanzibar kuja Bara alipe kodi, hii ni kero kubwa,"- Bakar Hamad

Mbunge.png
 
Kero ni Mzanzibari, kisiwa chenye idadi ya watu milioni 1, kuongoza Bara kwenye watu millioni 60. Tuanzie hapo kwanza.

hiyo kero inayowaathiri zaidi ni wabara, mana wao ndio wanaonunua vitu zanzibar na kupigwa ushuru hapa bandarini, Lakini kwa vile moyo wako tayari umeshajaa chuki unaishia kuongea pumba.
 
Wakisema waache kutoza Kodi Italeta mianya ya ukwepaji Kodi , kwamba hata wamalawi watapitisha mizigo Zanzibar wakisingizia umetoka Zanzibar kumbe la
Kuna mambo mengine hufanyika kwa sababu ya kukariri, uwezo mdogo wa kupambanua na kudhibiti hali kwa akili ya kawaida tu.

Vitu vya matumizi ya mtu mmoja mmoja haviathiri kodi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na faida ya kisiasa na umoja wa kitaifa kivitendo.
 
Kuna mambo mengine hufanyika kwa sababu ya kukariri, uwezo mdogo wa kupambanua na kudhibiti hali kwa akili ya kawaida tu. Vitu vya matumizi ya mtu mmoja mmoja haviathiri kodi kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na faida ya kisiasa na umoja wa kitaifa kivitendo.
Vitu vingi huanzia kwenye kimoja kimoja
Ukisamehe kimoja umesamehe vingi
 
Wakisema waache kutoza Kodi Italeta mianya ya ukwepaji Kodi , kwamba hata wamalawi watapitisha mizigo Zanzibar wakisingizia umetoka Zanzibar kumbe la
Mbona wapo waliokua wanasema mizigo inaenda Zambia au Malawi ilihali mafuta hayo hayo yakaishia kuuzwa maeneo ya mipakani Ili kukwepa Kodi Fulani Fulani maana mzigo ni transit. So wizi wa Kodi hautegemei msamaha wa Kodi huko zenji.
 
Haiwezekani mwananchi amesafiri kutoka Zanzibar na TV moja used anakuja kutumia nyumbani anafika Bara anaambiwa alipe kodi na hii ni nchi moja, akini anayetoka Morogoro kwenda Dar halipi kodi, lakini anayetoka Zanzibar kuja Bara alipe kodi, hii ni kero kubwa,"- Bakar Hamad

Sio Tv tu juzi Kuna mtu kabeba sukar kilo 5 kutoka unguja kufika bandarini anaambiwa eti either alipe faini au aiache sukar yake bandarini, yule msichana akawaambie chukueni mm Sina pesa wakajidai kumrudishia,

Na huyo mbunge angeongelea na issue ya kutoa mazao mfano ndizi kutoka bara kwenda Zanzibar refer case ya yule mama mjane aliyeporwa ndizi zake bandar ya Zanzibar wakapewa wafungwa
 
Hapana bnana kwa sukari kilo 5 sio kweli!!juzi juzi tu nimetoka unguja nimebeba kilo tano,na wengi tu walikuwa nazo cjaona hata mmoja akiulizwa juu ya kuilipia!!
 
Kero ni Mzanzibari, kisiwa chenye idadi ya watu milioni 1, kuongoza Bara kwenye watu millioni 60. Tuanzie hapo kwanza.
Mbona JPM katoka kawilaya kadogo ka Chato tena yenye watu chini ya laki moja halafu akaongoza wilaya zote zenye watu mil. 60. JK katoka wilaya ndogo ya Bagamoyo pia kaongoza wilaya zote. Mkapa katoka Kijiji cha Lupaso akaongoza vijiji vyote.
 
Unanunua bidhaa kutoka nchi nyingine kwanini usilipe Kodi? Wala hawakosei kukutwanga Kodi, Zanzibar Kuna raisi pale, hivyo Ile ni nchi.. ukileta bidhaa huku bara, tayari unakuwa umeingiza kwenye nchi nyingine ambayo ni Tanzania, maana huku nako Kuna raisi....
 
Back
Top Bottom