Mbunge Lijualikali ahojiwa na TAKUKURU. Adai wabunge wa CHADEMA wamejipanga kudanganya lakini hawatafanikiwa!


Nashukuru kwanza kwa kupoteza muda wako kusoma mchango wangu na kuujibu. Pia nashukuru kwa hizo sifa ulizonimwagia bila kujali kuwa ni za kweli au kinyume chake. Kuhusu hoja zako kwa kile kinachoendelea huko twitter, nitajibu kwa mtazamo kutokana na mtiririko wako wa namba.
  1. Mawazo kuhusu kuboresha hicho kipindi tumeshatoa kwa nyakati tofauti, labda ni wale wanaoratibu tu kuyafanyia kazi. Si vibaya ukitoa email ili tutume ushauri wetu huko.
  2. Ni kweli ww ni mtu critique na mkosoaji wa rais Magufuli, kwa id yako ya verified sioni ukiweza kwenda zaidi ya hapo, hasa kutokana na hali halisi. Ila unaposema eti ni mkosoaji mkubwa sio kweli. Huenda kuna namna ulitaka kusema ila unakosa maneno mazuri ya kuliweka. Lakini kusema ni mkosoaji mkubwa hilo sio kweli. Tena ww ni msifiaji kuliko ukosoaji, sina tatizo na hilo kwani ni haki yako.
  3. Paskali tuwe wakweli, viongozi wetu wa kiafrika ni nadra sana kufuata na kujirekebisha kwa ukosoaji au ushauri wa staha. Mfano mzuri na halisi ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Ni lugha au approach ipi ya staha haijatumika kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi? Hiyo katiba mpya iliyo pending, yenyewe ilifikiwa hatua iliyofikiwa baada ya cdm kufanya maandamano kadhaa. Hata katiba ya Zanzibar, ilipatikana baada ya machafuko. Hiyo ndio tabia yetu waafrika. Inaonekana hii propaganda ya kukosoa kwa lugha ya staha, imekuteka kiasi kwamba umeamini inahitajika lugha ya staha ili watu watii, jambo ambalo si kweli. Pepo hatolewi kwa lugha ya staha, bali hukemewa. Nikuhakikishei haya madai ya tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, iwapo kutatokea machafuko, ni lazima suluhu itapatikana, na sio lugha ya staha.
  4. Ni kweli kutundika mambo confidential ya serekali sio jambo jema, lakini unapata picha gani hayo mambo secret yanapokuwa ni ya nia ovu, dhidi ya watu wenye mitazamo mbadala dhidi ya serikali? Hiyo mipango ya serikali inawekwa hadharani kama sehemu ya watu wasioridhishwa na kukandamizwa na serikali, ili kuifanya serikali ijirekebishe. Tena njia hiyo ina afadhali, maana sehemu nyingine huwa na vikundi vya msituni kabisa.
  5. Sina hakika kama mimi Ni asset yoyote ndani ya nchi hii, kwani asset ndani ya nchi hii ni wale wanaosifia serikali na kumsifia rais. Mimi kwa mwenendo wangu, sio katika hizo asset.
 
Mhe. Lijualikali ametufahamisha kuwa Takukuru wanajua yote kuhusu pesa za Chadema na watakaodanganya hawatafanikiwa! Je, maneno haya Lijualikali aliambiwa na Takukuru? Kama alihojiwa haya maneno siyo mahojiano ni taarifa, Takukuru imuonye Lijualikali kwa kauli hii ili uchunguzi wake uaminike.
 
TAKUKURU = CCM
Lijualikali = CCM
 
TAKUKURU MTUAMBIE ILE TRILIONI 1.5 ALIYESEMA CAG MMEJUA ILIPOPELEKWA,MNAACHA UFISADI WA KUTISHA NAMNA HII UNAOUMIZA WANANCHI,MNAENDA KUPAMBANA NA CHADEMA CHAMA BINAFSI
 
Hao TAKUKURU wamepoteza "credibility" ya kuitwa ni chombo cha Umma.

Badala yake kingebadilishwa jina na kuitwa chombo kinachopokea maelekezo toka kwa Jiwe!

Unakumbuka wakati ule Mheshimiwa Nassari alipowakabidhi video clip, kuonyesha ushahidi wa wazi kabisa, namna aliyekuwa DC wa Aru Meru Mashariki, Alexander Mnyeti, anavyowanunua madiwani wa Chadema.........

Nini kilitokea baada ya kikabidhiwa ushahidi huo, ni kwa huyo mtuhumiwa kupandishwa cheo na kuwa RC mpya wa mkoa wa Manyara!
 
Huwezi fikia kiwango ambacho nimekuwa dissapointed na huyu mtoto Silinde. Nilikua najaribu kumuangalia kwa karibu kama mmoja wa vijana wa sasa wanaolwenda kuwa viongozi bora kabisa. Sijui ni kitu gani amekifanya huko gizani ambacho hatukijui wanakitumia dhidi yake.
 

Takukuru inafanya uchunguzi kutokana na kauli ambazo zimekuwa zinalalamikiwa na wabunge wanaoondoka
pia wanaangalia katiba yenu inasemaje kuhusu maamuzi na taratibu za matimizi ya pesa je yalikuwa yanafaata utaratibu?
kama yatakuwa sawa basi viongozi watakuwa sawa ila kama yanakiuka utaratibu kupitia kanuni na tratibu za katiba ya chama basi hilo litakuwa wazi kama wabunge walivyo lalamika.
Kwa hyo ni jambo liko wazi sana, maana kuja mjumbe wa kamati kuu hivi karibuni katoa na Accounts za chama kuwa zifuatiliwe, hivyo kila kitu kiko wazi
 
kuna factor ya urumi wake na wa mwenyekiti....... USIIPUUZE!...... usishangae next cabinet anakua waziri!


nilianza kuiona NGUVU hii factor baada ya Slaa kwenda kuungana na magufuli, huku Sumaye akienda kuungana na Lowassa!


ukitazama kwenye darubini unaona hivi vyama vimekaa kidini flan.... like wale ni waprotestant wakati sisi ni warumi!.......
 
Huyu mbona anahangsika Sana na chama alichotoka badala ya kusoma itikadi na falsafa ya chama chake kipya? Anawashwawashwa.
 
Nimewasikiliza baadhi yawabunge wa chadema waliohojiwa na takukuru kuhusu tuhuma za matumizi ya fedha za chama sijapata majibu ya maswari muhimu yaliyohojiwa na lijua likari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…