Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Mkuu Tindo, kwanza nianze kwa kukushukuru, much respect, pili nimefarijika sana na ukosoaji wako, ni very objective, nami pia nikiri no one is perfect, na mimi pia I'm only human.
Hoja yangu ya kilichoendelea Twitter ni was distasteful to some of us,
Watu kama wewe ni asset na ndio mnaweza kulisaidia taifa. Thanks for this.
- Kwanza asante kukifuatilia kipindi cha Jicho Letu, thanks for appreciation ya my inputs, tunaomba mawazo yenu ili tukiboreshe zaidi na zaidi.
- Humu jf mimi nimejibainisha ni mtu critique, mkosoaji mkubwa wa rais Magufuli lakini nakosoa responsibly
- Hivyo unaweza kukosoa responsibly kwa kutumia lugha za kistaarabu bila kutukana au lugha za kuudhi.
- Ku tundika secret documents za kuliaibisha taifa, hivyo pamoja na yote, tutumie mitandao responsibly kwa kutanguliza mbele utaifa
- Wewe Mkuu Tindo, you have the powers not only to read in between the lines, but to listen in between the words kwa kubaini thoughts of unspoken words, you are right on me!.
P
Nashukuru kwanza kwa kupoteza muda wako kusoma mchango wangu na kuujibu. Pia nashukuru kwa hizo sifa ulizonimwagia bila kujali kuwa ni za kweli au kinyume chake. Kuhusu hoja zako kwa kile kinachoendelea huko twitter, nitajibu kwa mtazamo kutokana na mtiririko wako wa namba.
- Mawazo kuhusu kuboresha hicho kipindi tumeshatoa kwa nyakati tofauti, labda ni wale wanaoratibu tu kuyafanyia kazi. Si vibaya ukitoa email ili tutume ushauri wetu huko.
- Ni kweli ww ni mtu critique na mkosoaji wa rais Magufuli, kwa id yako ya verified sioni ukiweza kwenda zaidi ya hapo, hasa kutokana na hali halisi. Ila unaposema eti ni mkosoaji mkubwa sio kweli. Huenda kuna namna ulitaka kusema ila unakosa maneno mazuri ya kuliweka. Lakini kusema ni mkosoaji mkubwa hilo sio kweli. Tena ww ni msifiaji kuliko ukosoaji, sina tatizo na hilo kwani ni haki yako.
- Paskali tuwe wakweli, viongozi wetu wa kiafrika ni nadra sana kufuata na kujirekebisha kwa ukosoaji au ushauri wa staha. Mfano mzuri na halisi ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Ni lugha au approach ipi ya staha haijatumika kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi? Hiyo katiba mpya iliyo pending, yenyewe ilifikiwa hatua iliyofikiwa baada ya cdm kufanya maandamano kadhaa. Hata katiba ya Zanzibar, ilipatikana baada ya machafuko. Hiyo ndio tabia yetu waafrika. Inaonekana hii propaganda ya kukosoa kwa lugha ya staha, imekuteka kiasi kwamba umeamini inahitajika lugha ya staha ili watu watii, jambo ambalo si kweli. Pepo hatolewi kwa lugha ya staha, bali hukemewa. Nikuhakikishei haya madai ya tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, iwapo kutatokea machafuko, ni lazima suluhu itapatikana, na sio lugha ya staha.
- Ni kweli kutundika mambo confidential ya serekali sio jambo jema, lakini unapata picha gani hayo mambo secret yanapokuwa ni ya nia ovu, dhidi ya watu wenye mitazamo mbadala dhidi ya serikali? Hiyo mipango ya serikali inawekwa hadharani kama sehemu ya watu wasioridhishwa na kukandamizwa na serikali, ili kuifanya serikali ijirekebishe. Tena njia hiyo ina afadhali, maana sehemu nyingine huwa na vikundi vya msituni kabisa.
- Sina hakika kama mimi Ni asset yoyote ndani ya nchi hii, kwani asset ndani ya nchi hii ni wale wanaosifia serikali na kumsifia rais. Mimi kwa mwenendo wangu, sio katika hizo asset.