Mbunge Lijualikali ahojiwa na TAKUKURU. Adai wabunge wa CHADEMA wamejipanga kudanganya lakini hawatafanikiwa!

Mbunge Lijualikali ahojiwa na TAKUKURU. Adai wabunge wa CHADEMA wamejipanga kudanganya lakini hawatafanikiwa!

Mkuu Tindo, kwanza nianze kwa kukushukuru, much respect, pili nimefarijika sana na ukosoaji wako, ni very objective, nami pia nikiri no one is perfect, na mimi pia I'm only human.

Hoja yangu ya kilichoendelea Twitter ni was distasteful to some of us,
  1. Kwanza asante kukifuatilia kipindi cha Jicho Letu, thanks for appreciation ya my inputs, tunaomba mawazo yenu ili tukiboreshe zaidi na zaidi.
  2. Humu jf mimi nimejibainisha ni mtu critique, mkosoaji mkubwa wa rais Magufuli lakini nakosoa responsibly
  3. Hivyo unaweza kukosoa responsibly kwa kutumia lugha za kistaarabu bila kutukana au lugha za kuudhi.
  4. Ku tundika secret documents za kuliaibisha taifa, hivyo pamoja na yote, tutumie mitandao responsibly kwa kutanguliza mbele utaifa
  5. Wewe Mkuu Tindo, you have the powers not only to read in between the lines, but to listen in between the words kwa kubaini thoughts of unspoken words, you are right on me!.
Watu kama wewe ni asset na ndio mnaweza kulisaidia taifa. Thanks for this.
P

Nashukuru kwanza kwa kupoteza muda wako kusoma mchango wangu na kuujibu. Pia nashukuru kwa hizo sifa ulizonimwagia bila kujali kuwa ni za kweli au kinyume chake. Kuhusu hoja zako kwa kile kinachoendelea huko twitter, nitajibu kwa mtazamo kutokana na mtiririko wako wa namba.
  1. Mawazo kuhusu kuboresha hicho kipindi tumeshatoa kwa nyakati tofauti, labda ni wale wanaoratibu tu kuyafanyia kazi. Si vibaya ukitoa email ili tutume ushauri wetu huko.
  2. Ni kweli ww ni mtu critique na mkosoaji wa rais Magufuli, kwa id yako ya verified sioni ukiweza kwenda zaidi ya hapo, hasa kutokana na hali halisi. Ila unaposema eti ni mkosoaji mkubwa sio kweli. Huenda kuna namna ulitaka kusema ila unakosa maneno mazuri ya kuliweka. Lakini kusema ni mkosoaji mkubwa hilo sio kweli. Tena ww ni msifiaji kuliko ukosoaji, sina tatizo na hilo kwani ni haki yako.
  3. Paskali tuwe wakweli, viongozi wetu wa kiafrika ni nadra sana kufuata na kujirekebisha kwa ukosoaji au ushauri wa staha. Mfano mzuri na halisi ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Ni lugha au approach ipi ya staha haijatumika kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi? Hiyo katiba mpya iliyo pending, yenyewe ilifikiwa hatua iliyofikiwa baada ya cdm kufanya maandamano kadhaa. Hata katiba ya Zanzibar, ilipatikana baada ya machafuko. Hiyo ndio tabia yetu waafrika. Inaonekana hii propaganda ya kukosoa kwa lugha ya staha, imekuteka kiasi kwamba umeamini inahitajika lugha ya staha ili watu watii, jambo ambalo si kweli. Pepo hatolewi kwa lugha ya staha, bali hukemewa. Nikuhakikishei haya madai ya tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, iwapo kutatokea machafuko, ni lazima suluhu itapatikana, na sio lugha ya staha.
  4. Ni kweli kutundika mambo confidential ya serekali sio jambo jema, lakini unapata picha gani hayo mambo secret yanapokuwa ni ya nia ovu, dhidi ya watu wenye mitazamo mbadala dhidi ya serikali? Hiyo mipango ya serikali inawekwa hadharani kama sehemu ya watu wasioridhishwa na kukandamizwa na serikali, ili kuifanya serikali ijirekebishe. Tena njia hiyo ina afadhali, maana sehemu nyingine huwa na vikundi vya msituni kabisa.
  5. Sina hakika kama mimi Ni asset yoyote ndani ya nchi hii, kwani asset ndani ya nchi hii ni wale wanaosifia serikali na kumsifia rais. Mimi kwa mwenendo wangu, sio katika hizo asset.
 
Mhe. Lijualikali ametufahamisha kuwa Takukuru wanajua yote kuhusu pesa za Chadema na watakaodanganya hawatafanikiwa! Je, maneno haya Lijualikali aliambiwa na Takukuru? Kama alihojiwa haya maneno siyo mahojiano ni taarifa, Takukuru imuonye Lijualikali kwa kauli hii ili uchunguzi wake uaminike.
 
Mhe. Lijualikali ametufahamisha kuwa Takukuru wanajua yote kuhusu pesa za Chadema na watakaodanganya hawatafanikiwa! Je, maneno haya Lijualikali aliambiwa na Takukuru? Kama alihojiwa haya maneno siyo mahojiano ni taarifa, Takukuru imuonye Lijualikali kwa kauli hii ili uchunguzi wake uaminike.
TAKUKURU = CCM
Lijualikali = CCM
 
Mbunge wa Kilombero mh Lijualikali alikuwa ni miongoni mwa wabunge wa Chadema waliohojiwa na Takukuru kuhusiana na matumizi ya fedha za chama.

Baada ya kuhojiwa mh Lijualikali aliongea na waandishi wa habari na kuwaambia mahojiano yake na Takukuru yamefanyika vizuri.

Zaidi akasema ana taarifa kuwa wabunge wa Chadema wamejipanga ili kutoa taarifa za uwongo na kumnusuru Mbowe.

Lijualikali ameapa kuwa wabunge hao hawatafanikiwa katika njama walizopanga.

Chanzo: Eatv habari

Maendeleo hayana vyama!
TAKUKURU MTUAMBIE ILE TRILIONI 1.5 ALIYESEMA CAG MMEJUA ILIPOPELEKWA,MNAACHA UFISADI WA KUTISHA NAMNA HII UNAOUMIZA WANANCHI,MNAENDA KUPAMBANA NA CHADEMA CHAMA BINAFSI
 
Mhe. Lijualikali ametufahamisha kuwa Takukuru wanajua yote kuhusu pesa za Chadema na watakaodanganya hawatafanikiwa! Je, maneno haya Lijualikali aliambiwa na Takukuru? Kama alihojiwa haya maneno siyo mahojiano ni taarifa, Takukuru imuonye Lijualikali kwa kauli hii ili uchunguzi wake uaminike.
Hao TAKUKURU wamepoteza "credibility" ya kuitwa ni chombo cha Umma.

Badala yake kingebadilishwa jina na kuitwa chombo kinachopokea maelekezo toka kwa Jiwe!

Unakumbuka wakati ule Mheshimiwa Nassari alipowakabidhi video clip, kuonyesha ushahidi wa wazi kabisa, namna aliyekuwa DC wa Aru Meru Mashariki, Alexander Mnyeti, anavyowanunua madiwani wa Chadema.........

Nini kilitokea baada ya kikabidhiwa ushahidi huo, ni kwa huyo mtuhumiwa kupandishwa cheo na kuwa RC mpya wa mkoa wa Manyara!
 
Dr Slaa, Zito, Kitila hawa wote walikua vigogo ndani ya chadema lakini wameondoka bila kulalamikia ufujaji pesa pale cdm

Hawa vijana walioondoka awamu hii ya Magufuli sijui wamejifunza wapi kutukana waliowatoa jalalani.

Lijualikali simfahamu, lakn Silinde ameni-disappoint sana jamani, nilikua namwona kama very matured!
Huwezi fikia kiwango ambacho nimekuwa dissapointed na huyu mtoto Silinde. Nilikua najaribu kumuangalia kwa karibu kama mmoja wa vijana wa sasa wanaolwenda kuwa viongozi bora kabisa. Sijui ni kitu gani amekifanya huko gizani ambacho hatukijui wanakitumia dhidi yake.
 
Uchunguzi unapofanyika si sahihi baadhi ya waliochunguzwa kutoa muelekeo wa matokeo ya uchunguzi, hii inaleta picha kuwa matokeo tayari yamepangwa, nadhani Takukuru alitakiwa kuwatahadharisha wahojiwa wote kutotoa kauli za mahojiano. Kwa bali ilivyo inaonesha kuwa Takukuru iko upande mmoja, Lijualikali amejuaje yaliyoko upande wa Takukuru kuwa inajua kilakitu? Refa anashirikiana na wachezaji wa upande mmoja.

Takukuru inafanya uchunguzi kutokana na kauli ambazo zimekuwa zinalalamikiwa na wabunge wanaoondoka
pia wanaangalia katiba yenu inasemaje kuhusu maamuzi na taratibu za matimizi ya pesa je yalikuwa yanafaata utaratibu?
kama yatakuwa sawa basi viongozi watakuwa sawa ila kama yanakiuka utaratibu kupitia kanuni na tratibu za katiba ya chama basi hilo litakuwa wazi kama wabunge walivyo lalamika.
Kwa hyo ni jambo liko wazi sana, maana kuja mjumbe wa kamati kuu hivi karibuni katoa na Accounts za chama kuwa zifuatiliwe, hivyo kila kitu kiko wazi
 
Huwezi fikia kiwango ambacho nimekuwa dissapointed na huyu mtoto Silinde. Nilikua najaribu kumuangalia kwa karibu kama mmoja wa vijana wa sasa wanaolwenda kuwa viongozi bora kabisa. Sijui ni kitu gani amekifanya huko gizani ambacho hatukijui wanakitumia dhidi yake.
kuna factor ya urumi wake na wa mwenyekiti....... USIIPUUZE!...... usishangae next cabinet anakua waziri!


nilianza kuiona NGUVU hii factor baada ya Slaa kwenda kuungana na magufuli, huku Sumaye akienda kuungana na Lowassa!


ukitazama kwenye darubini unaona hivi vyama vimekaa kidini flan.... like wale ni waprotestant wakati sisi ni warumi!.......
 
Huyu mbona anahangsika Sana na chama alichotoka badala ya kusoma itikadi na falsafa ya chama chake kipya? Anawashwawashwa.
 
Nimewasikiliza baadhi yawabunge wa chadema waliohojiwa na takukuru kuhusu tuhuma za matumizi ya fedha za chama sijapata majibu ya maswari muhimu yaliyohojiwa na lijua likari.
 
Back
Top Bottom