Yeah, Mimi Ni mdau mkubwa wa hicho kipindi cha jicho letu ndani ya habari, tena sio kwa hizi promo zako ulioanza juzi humu jukwaani, bali ni kabla hata ya awamu hii ya tano kuingia madarakani. Nashukuru kwa siku za karibuni kwa ushawishi wako, umeongeza hamasa na watazamaji toka jf, kwa hili nakupongeza.
Paskali ulichozungumza kwenye kipindi kile kuhusu twitter nilikisikia, sitaki kujiweka kwenye mitazamo ya wengi walisikia nini, lakini mtiririko wako ilikuwa ni kuwa ndani ya twitter kuna michango inakukwaza, na inakukwaza sio kwakuwa ni wakosaji sana, bali kuna mtu au watu kadhaa wainaikosoa serikali bila staha au vyovyote utakavyoiweka ww.
Ni wazi ulikuwa negative kwa mwenendo wa michango ya watu kadhaa wa twitter dhidi vya serikali, na ulifikia hitimisho la twitter kuchukuliwa hatua, kwa ww kujiweka kwenye kundi la huu uzalendo academia, for the reason best known to you. Unaweza kutumia utetezi wowote uutakao maana ni haki yako, lakini hivyo ndio nilivyokuelewa na sina shaka na hilo.