Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
MATARAJIO YA WAASISI WA CCM vs. KINACHOENDELEA
________________________
"Tunataka kuona katika Taifa hili, vijana jeuri na wenye kujiamini, si vijana waoga, akina "ndiyo bwana mkubwa", vijana wanaohoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya kitanzania. Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa" Mwl J.K. Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania.
Kufuatia Kitendo Cha Mpina Kumtuhumu Waziri wa Kilimo kwamba amelidanganya Bunge na kwenda Mbali zaidi kwamba amefanya utafiti na kupata ushahidi wa tuhuma hizo hilo ni jambo linaloonesha kwanza ndani ya CCM Kuna Demokrasia isipokuwa tu Kuna watu ndani ya Chama hawataki na hawapendi hilo litokee, wangependa mambo yaende kimya kimya, wananchi wasijue kinachoendelea.
Kwa maoni yangu Mpina ni miongoni mwa vijana ambao Mwl. Nyerere alikuwa anatamani Tanzania iwe nao.
Kwa akili ya kawaida kwa sisi wanaCCM wa kawaida tunaweza kusema Mpina anataka kuvuruga Chama na anataka kuivuruga Serikali.
Lakini kwa kurejea tu Katiba ya Chama ya mwaka 1977 ibara ya 5 kifungu Cha 7(a) inaeleza malengo ya Chama ni pamoja na "Kusimamia HAKI na MAENDELEO ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea"
Sasa Mpina alichofanya ni kusimamia na kutetea haki na Maendeleo ambapo kulingana na utafiti alioufanya kumeonekana kuna chembe chembe za kuhujumu Maendeleo.
Ukizingatia kazi na wajibu wa kibunge kama muwakilishi wa wananchi ni pamoja na kusimamia maslahi ya Taifa na kukemea vikali masuala yanayokwenda kinyume na Katiba, Kinyume na matarajio na malengo ya Chama ( CCM) na kisha kuyawasilisha kwa chombo husika na muhimu sana kuwapa mrejesho waliokutuma kuwawakilisha kazi uliyoifanya.
Huo ni wajibu wa msingi kabisa hasa kwa kuzingatia katiba ya Nchi Yetu. Chama kinapaswa kujivunia kwa kuwa na wabunge wa namna hii, Karne ya Sasa na Maendeleo yanavyokwenda kasi tunahitaji watu wa facts na evidence na sio brah brah.
Hii itasaidia Chama kupambana na vyama vingine ambavyo vinaendelea kuwajenga vijana Katika udadisi, kuhoji, kuwa na jeuri ya kupinga vitendo vya kuhujumu Maendeleo na kupora haki za wanyonge pasipo kuogopa.
Ccm ina misingi mizuri kama tu misingi hiyo itafuatwa kwa kunyooka na kuenzi matarajio ya Waasisi wa Chama ya kuwa na Chama Chenye vijana Shupavu, wenye uwezo wa kupambana na vitendo vya kinyonyaji, wizi na Ufisadi.