Mbunge, Maganga: TFS ni 'Disaster' kubwa, inakwamisha Biashara ya Kaboni, Waziri chukua hatua!

Mbunge, Maganga: TFS ni 'Disaster' kubwa, inakwamisha Biashara ya Kaboni, Waziri chukua hatua!

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mbunge wa Katavi, Thomas Maganga, amechangia hoja ya bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), leo Aprili 21, 2026, ambapo ameeleza changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa mipango ya mazingira na hasa biashara ya kaboni katika halmashauri mbalimbali nchini.

Akizungumza bungeni, Maganga amesema halmashauri nyingi zimejipanga kuingia kwenye biashara ya kaboni lakini zinakwamishwa na baadhi ya taasisi za serikali. Amesema tatizo kubwa linatokana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), akidai kuwa wamechukua maeneo mengi ya misitu na kuweka tangazo la Serikali (GN) kila kijiji, hali anayoieleza kuwa inachangia migongano ya matumizi ya ardhi.

"Sasa tukijipanga kuingia kwenye biashara ya kaboni, huku unakuta kuna zuio la NEMC. Mheshimiwa Mwenyekiti, haikubaliki! Na hawa TFS si kwamba wanakataa sisi tusiingie kwenye biashara ya kaboni kwa kuwa wanafaidika na hii misitu, hapana."

"Ukienda sasa hivi kwenye halmashauri zetu kuna contradiction (mgongano) kati ya TAWA na TFS. TAWA wanahifadhi misitu, TFS wanakata misitu! Leo Rais Samia anapiga magoti kupanda miti, alafu huku kuna taasisi ya serikali kazi yake ni kukata miti!"

"Naomba sana serikali na Mheshimiwa Waziri uje na majibu; ni lini NEMC itakuwa mamlaka kamili? Mheshimiwa Waziri usipokuja na haya majibu... shemeji yangu alikuwa pale juu, shemeji naondoka na mshahara wa mzee! Bila majibu ya lini NEMC itakuwa mamlaka, mimi napita na mshahara bila kujali matatizo yatakayotokea!"

 
Back
Top Bottom