Mbunge Mavunde Akabidhi Uwanja wa Michezo wa Kisasa Shule ya Sekondari K/Ndege Dodoma

Mbunge Mavunde Akabidhi Uwanja wa Michezo wa Kisasa Shule ya Sekondari K/Ndege Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Ni wa michezo ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amekabidhi kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege kiwanja cha kisasa cha michezo ya mpira wa kikapu,pete na wavu kama sehemu ya kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wa Jijini Dodoma.
WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.42.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.42(1).jpeg

Tukio hilo limefanyika jana tarehe 2/11/2024 katika shule ya sekondari ya Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma .

“Namshukuru sana Mh.Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kuboresha miundombinu ya mazingira rafiki ya kusomea kwa shule zetu nyingi ikiwemo Shule ya sekondari Kiwanja cha Ndege.

Katika kuunga mkono jitihada hizi kubwa nimeamua kujenga uwanja huu wa kisasa wa michezo hapa shuleni ili kusaidia kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wa Dodoma”Alisema Mavunde
WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.43.jpeg

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mh. Alhaj Jabir Shekimweri amempongeza Mbunge Mavunde kwa juhudi kubwa ya kuleta maendeleo Jijini Dodoma na kuwataka wanafunzi kutumia kiwanja kushiriki kwenye michezo ili kujenga Afya bora hali itakayowasaidia kujiepusha na makundi mbalimbali ambayo yataathiri maadili yao na afya.
WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.43(1).jpeg

Akitoa salamu zake, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchini(TBF) Ndg. Michael Kadebe amepongeza juu ya ujenzi wa kiwanja hicho kwa kuwa inaongeza idadi ya viwanja vya Mpira wa Kikapu Jijini Dodoma na kuahidi kuanzisha kituo cha mafunzo ya vijana MAVUNDE BASKETBALL ACADEMY katika shule hiyo kama njia ya kuwaendeleza wanafunzi katika ushiriki wao kwenye mchezo wa kikapu Jijini Dodoma.
WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.43(2).jpeg
WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.44(1).jpeg

Wakitoa salamu za Shukrani Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Mh. Amos Mbaranga na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule Ndg. Bryson Lema wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa ujenzi wa kiwanja katika Shule hiyo ambacho kimebadilisha muonekano wa shule hiyo kimazingira na ambacho kitachochea kuwaandaa wanamichezo wa baadaye na tegemeo la Taifa kupitia shule hiyo huku wakiahidi kukitunza kiwanja hicho kwa hali na mali ili kiwafae kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.45(2).jpeg
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.44.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.44.jpeg
    249.4 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.45.jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.45.jpeg
    123.5 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.45(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-11-03 at 12.28.45(1).jpeg
    118.3 KB · Views: 5
Back
Top Bottom