Mbunge: Mbowe alidanganya Watanzania, Biashara zake hazikufungwa na Serikali bali Wanafamilia yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Viti Maalum kutoka CCM, Jackline Ngonyani, amesema Mwenyekiti wa CHADEMA aliwadanganya Watanzania kuhusu Serikali kufunga biashara zake na kumyanyasa.

Amesema biashara anazozifanya Mbowe ni za urithi wa Familia na alikuwa anazifanya bila kuwapa mrejesho Wanafamilia ndipo walipokwenda Mahakamani na Mahakama kuamuru kumzuia kuendelea na biashara hizo.

Aidha, amesema Jengo la Billcanass lilichukuliwa kutokana na Mbowe kutokulipa kodi kwa muda mrefu kwasababu lile ni jengo la Serikali.

 
Asema pia alidanganya amefungwa.
 
Sijui ni nani aliyetoa wazo la kuivunja billcanas mi moja ya wazo bovu kufanywa tokea ile siku ndipo nilijua kuwa tz hatuna mipango bali siasa chafu unavunja asset ambayo waliweza kumpangisha mtu wao wakaona bola wavunje ili wazungushe mabati na pesa wakose[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Mbowe amezoea kuishi kwa uwongo anawadanganya wajinga pale ufipa ila ccm haiwezi
 
Hao ndio wanaosema hakuharibiwa bustani zake.,hakufungwa,hakufungiwa biashara.
 
Mbaya zaidi hilo jengo lilijengwa na baba yake Mbowe, Nyerere alilitaifisha akawapa NHC.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…