Watu wenye akili za kibaguzi hata wakiwa wabunge hawasahau asili yao. Yeye alipoingia huku Tanganyika ameingia kwa passport? Ila sishangai sana maana watu au Mtu mbinafsi siku zote dalili yake ya kwanza huwa ni hii
“Chako ni chetu sote lakini chake ni chake peke yake”
 
Nasemaje...! Zanzibar asiachwe, hiyo ndoa akae akijua ni ya hadi dahari!

Na ikiwezekana, Zanzibar iachwe kuwa huru kwa siku tatu halafu itekwe na kulazimishwa kuwa nchi moja ambayo itakuwa na Rais mmoja tu

Hakuna tena sjui cha serikali ya wapi na wapi
 
Zanzibar ni nchi Passport muhimu 🐼
 
Sio wazo baya mradi tu wazanzibari nao waingie bara kwa hati za kusafiria. Nao wapewe muda wa kuishi bara kulingana na kibali chao cha kuingia nchi nyingine ya bara. Hii ni kwa sababu ardhi imekwisha Bara. Nchi iliyokuwa na watu hawafiki milioni 10 wakati wa Muungano sasa hivi tunanusa milioni 70. Ardhi iliyopo haitutoshi kwa kweli.

Na wasiruhusiwe kuchukua mchanga wa bara kwa sababu wanatuharibia mazingira. Hata ajira wapewe kwa vibali maalum kwa sababu ni lazima tulinde ajira kwa ajili ya vijana wetu.

Huyu Mheshimiwa anahitaji kupewa shukrani kwa kweli. Ni wazo zuri sana.

Amandla....
 
Tanganyika ilipewa kazi maalumu na US Zanzibar Isiwe huru hatadakika Moja.Ndio maana wakati wa mwalimu ukizungumzia muungano Yanakukuta🤣🤣🤣.
Hata Aboudu jumbe Raisi baada ya karume yalimkuta.
US ina interest ipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…