Mbunge Musukuma aambiwe kuwa pesa sio mbadala wa elimu

Hawezi kujua umuhimu wa elimu maana hakuipata.
 
Elimu wakati una njaa ni sawa na kiingereza bila ela.
Kama umesomana hujaweza kutatua changamoto zako za kila siku za uhakika wa kula, na mahitaji ya msingi, hiyo elimu haina maana ni sawa huna elimu.
 
Pesa haina mbadala wala elimu haina mbadala, hivyo kila kitu kinasimama katika nafasi yake.
Mimi nilidhani unatupa mbadala wa pesa kama pesa sio mbadala wa elimu basi mbadala
 
Hawezi kukua umuhimu wa elimu maana hakuipata.
Elimu isiyo badili maisha ya mtu haina maana!
Kazi ya elimu ni kukupa mwanga ili iweze kuyatawala mazingira!
Mimi naamini hakuna mtu mwenye pesa hana elimu ya maisha ambayo ni muhimu zaidi kuliko elimu hizi za kusoma masomo mengi yasiyokufanya kupata pesa!
 
Sijui kwann watanzania wengi wanachukulia elimu poa sana..lkn hakuna Taifa linaweza endelea bila kuwa na elimu..ata kama haijatunufaisha kama nchi inabidi turudi on the drawing board na kurestructure elimu yetu na namna itatunufaisha kama Taifa...badala ya kuendelea na debates uchwara za shule ya msingi education vs money..haisadii kitu
 

Unamchosha bure tu Kichuguu, bora ungekuwa mpole ujifunze kutoka kwake.

Lengo la elimu siyo utajiri wala ajira.
 
Tatizo humu kuna watu wengi mnajifanya wajuaji. Ni vizuri kuuliza zaidi ili kujifunza.
 
Elimu yetu inakosa maana kwa sababu haina maarifa ndani yake!
Kwa sehemu kubwa ni kusoma makaratasi tu ila skills ni ndogo sana!
Wenzetu Wachina elimu yao imelenga kuyatawala mazingira ila ya kwetu ngoja liende!
Elimu ya Tanzania japo kweli kuna baadhi imewapa maisha na connection ila kwa sehemu kubwa ni miyeyusho na kuambulia kufanya kazi kama vibarua tu!
 
Tatizo humu kuna watu wengi mnajifanya wajuaji. Ni vizuri kuuliza zaidi ili kujifunza.
Wewe usijifanye unajua sana! Elimu hii ya Kitanzania ndo maana inahojiwa!
Ila hatima ya elimu uweze kuwa na kipato na kutawala mazingira kama unaona wewe elimu ina umuhimu tofauti na niliyotaja hapo sema!
Watanzania wengi wana elimu ila hawana maarifa hapo ndo tujiulize kwa nini elimu haitoi matokeo!
Ukitaka kuona wasomi wa kibongo kuwa bado saba na elimu haijawasaidia angalia huduma wanazotoa ni Very poor!
 
Ata kuwa kinyozi ni elimu tatizo tz ni kuona elimu ni ya university tu
 
Ana mantiki ambayo nafikiri hujaelewa, hata Marehemu Magufuli aliwahi kusema pamoja na kuteua PhD kibao kwenye wizara mojawapo, msaada au matokeo yalikua hasi. Anachochallenge Msukuma sio elimu kukosa faida, ila output za wenye elimu kwenye taasisi za umma. Mfano, kampuni za mabasi hata daladala, tena nyingi wamiliki hawana elimu zina ongeza mabasi kila mwaka na wanakopa benki, ww msomi unapewa 300 sio mkopo, njia za upendeleo, bado mabasi yana kufa alafu unatuambia una elimu, ya nini sisi?
 
Jana nimemsikiliza msukuma
Kuna engo naona hujaigusia
 
Mkuu una hoja nzito sana. Kuhusu skills nakuunga mkono 100%. Shati lililoshonwa na fundi Juma wa Mburahati na shati lililoshonwa na Mchina wa Guangzhou ni product moja yenye mionekano miwili tofauti ingawa wametumia mashine sawa. Majamaa wanatuzidi skills sana. Ninachopinga ni kuona elimu haina maana. Ninadhani elimu yetu iboreshwe ili kutoa skilled labour.
 
Unamchosha bure tu Kichuguu, bora ungekuwa mpole ujifunze kutoka kwake.

Lengo la elimu siyo utajiri wala ajira.
Lengo la elimu ni nini kuondoa ujinga sawa halafu baada ya kuondoa ujinga nini kinafuata unaajiriwa au unajiajiri kutokana na elimu uliyonayo kuondoa changamoto baada ya kupata ajira unafanya kazi kuendana na taaluma unapewa Check Number yako kila mwisho wa mwezi unalipwa kiasi chako unaanza kujiendeleza kimaisha si ndio au wewe mtazamo wako upo wapi?

Unarudi palepale unapata elimu ili update ujuzi fulani kisha baada ya kupata huo ujuzi uutumie huo ujuzi ulioupata kufanya kazi na kujiingizia pesa au wewe una maana nyingine ya elimu na ujuzi?

Unaona unaporudi kwa hio wewe mtoto/watoto wako unawapeleka shule wakapate elimu na ujuzi ili waondokane na ujinga, wakashangae majengo au unawasomesha ili baadae waweze kupata kazi zinazoendana na ujuzi wao na kutengeneza pesa na kujitegemea wenyewe? Au wewe unawapeleka shule watoto wako wakapate elimu na ujuzi km fashion? Au wewe unawapeleka shule watoto wako wakasome sababu serikali inakulazimisha kufanya hivyo? Which is which?
 
nilimsikiliza mwanzo mwisho mtoa mada wewe ndio unapotosha alichoongea

hakuna mahali alisema anadharau elimu isipokuwa anadharau pale anapoona watu waliodhaniwa wameelika kutenda mambo ya kipuuzi makazini kuliko hata hao ambao hawajasoma

elimu imkomboe mtu na si kuonekana amesoma wakati hana maalifa aliyoenda kuyasomea
 
Mbona mi namsikilizaga mara nyingi, sikumbuki kama nimewahi kumsikia akibeza elimu, namsikia mara nyingi akiwabeza wasomi na sio elimu. Msukuma angekua anabeza elimu, asingekua ana support elimu jimboni kwake, asingepeleka watoto wake shule. Kuna kubeza elimu na kubeza wasomi, kuna tofouti hapo.
 
Sasa kuna fundi mchundo hapo anasema hausomi ili upate pesa ili uajiriwe ili upate kazi kwa hio wale wanaoajiriwa wanafanya kazi bure si wanaingiza pesa kila mwisho wa mwezi?

Mfumo wa elimu yetu tuliyonayo kuanzia msingi mpaka chuo kikuu ni ya kumtengeneza mwanafunzi msomi kua mwajiriwa mindset yake inatengenezwa kwamba akimaliza kusoma ajira na kazi vipo mlangoni kwake kuanzia chini yaan hufundishwi kua mtu wa kujiajiri then kuna mtu anakwambia kwamba elimu yetu hailengi watu kusoma ili waajiriwe au wapate kazi na kutengeneza pesa who said that?

Sasa baada ya elimu nini kinafuata? Usizungumzie tu elimu kisha ukabakia hapo hapo what is next after that? Sawa una elimu nini kinafuata baada ya kuelimika umeshasoma umepata ujuzi umefuzu mafunzo nini kinafuata ukae tu na kujisifu mimi nimesoma na mfukoni huna pesa? Watu watakuona Fala na elimu yako una elimu halafu huna kazi huna ajira huna pesa unaonekana bogus tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…