Mbunge Nchambi na wenzake 2 wakiri makosa ya uhujumu uchumi na kulipa faini

Mbunge Nchambi na wenzake 2 wakiri makosa ya uhujumu uchumi na kulipa faini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Nchambi.jpeg

Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Suleiman Masoud Nchambi (CCM), pamoja na wenzake wawili wamekiri makosa dhidi ya kesi iliyokuwa ikiwakabili ya Uhujumu Uchumi, na kuamuliwa kulipa faini kila mmoja au kwenda Jela, ambapo wote wamelipa faini na kuachiwa huru.

i/ Nchambi amekabilia na makosa 9 na kutakiwa kulipa Shilingi Milioni 22.5.

ii/ Yahya Soud amekabiliwa na makosa 4 amelipa Shilingi Milioni 7.

iii/ Abdala Soud, makosa 2, amelipa Shilingi Milioni 3.

Pia soma
- Mbunge wa Kishapu, Suleiman Nchambi (CCM) mbaroni kwa kukutwa na Silaha 16 na risasi 536

- Mbunge wa Kishapu(CCM), Suleiman Nchambi aliyekutwa na silaha 16 aburuzwa mahakamani, asomewa mashitaka 12
 
Nakumbuka jinsi ilivyokuwa akimponda Salome Makamba kuhusu wachimbaji wadogo kule Mwadui. Yaani Nchambi alijionyesha kama kada kindandaki wa CCM Bungeni kumbe usiku ni mhujumu mkubwa wa uchumi na jangili. Ile kaulimbiu weka mbali na tembo inafaa kutumika kwa huyu jamaa.

Vv
 
Milioni 32.5 kibindoni hazina.

Penye udhia penyeza rupua Maisha yanaendelea.
 
Dah..hata kiinua mgongo hakijatikisika kabisa...

Sasa na yale mabunduki wanamrudishia au?

Kwanini asirudishiwe wakati keshalipa fine? kweni mdogo wake Rostam kesi yake ya silaha kama huyu iliishaje?
 
Hii serikali inaelekea kufilisika bila shaka! Jangili sugu kama hilo linalipa faini ili iweje sasa! Lilitakiwa lifungwe miaka mingi gerezani na mali zake zote kufilisiwa.

Halafu chakushangaza Majangili na Mafisadi yote yanafungamana na Ccm! Utakuta ni Wabunge au Wachina!! Hii Ccm ifikie wakati ituachie Nchi yetu.
 
Back
Top Bottom