Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
"Mgogoro wa Ardhi baina ya kijiji cha Rusumo na Gereza la Rusumo, mgogoro ulioletwa na Afisa wa Ardhi ambaye Mamlaka yake ya kinidhamu yapo chini ya Wizara ya Ardhi." - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Afisa kwa kushirikiana na viongozi wa Gereza la Rusumo walikwenda wakajifungia kwenye chumba wakachukua Laptop + Mause na Software wakaanza ku generate Coordinate wakapima eneo linalomilikiwa na Gereza" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Matokeo yake, Coordinate ya kwanza yaliangukia kwenye mto tunaoumiliki Tanzania na Taifa lingine. Coordinate nyingine iliangukia eneo linalomilikiwa na TANAPA. Coordinate nyingine iliangukia kwenye barabara ya kimataifa iliyokuwepo kabla ya Gereza kuwepo. Matokeo yake wametuletea matatizo makubwa sana" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Kanali Mathias Kahabi aliunda tume ya kuchunguza, tulitumia kifaa kinachoitwa Real Time Kinematics (RTK) kwa ajili ya ku verify. Nimeshamuambia Masauni, wanampotosha Magereza. Ninaomba Wizara ya Ardhi mshughulike na huyu Afisa Ardhi ambaye ametuletea matatizo" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Jambo la mwaka 2025 limeshakaa vizuri maeneo mengi, naomba msiniharibie. Mgogoro huu muende muondoe mara moja kwa sababu kitu kimeshakaa kibla 2025 nataka nipite kwa kuogelea" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Eneo lingine ninalotaka kuchangia ni Namna Wizara ya Ardhi inafanya utafiti wa kujua Viwango vya Fidia kwenye maeneo mbalimbali nchini. Ngara kuna mchakato wa disclosure unaendelea ambapo mthamini Mkuu wa Serikali ameusimamia" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Mama mmoja Mrs Zuhura Hillary aliachiwa nyumba na baba yake mwaka 1943. Hii nyumba wameifanyia uthamini wanataka kumlipa Shilingi Laki Saba. Mama huyu aliachiwa nyumba na mume wake mwaka 1950 wanataka kumlipa Shilingi Milioni Moja na Laki Mbili. Hiyo fedha haitoshi kujenga banda la Kuku. Mama amesema bomoeni maeneo, majumba, na kila kitu mkachukue, hahitaji fedha maana haiendani kwa sababu haina uhalisia" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro
"Nimezungumza na mthamini Mkuu wa Serikali, utaratibu huu wa kuibua viwango vya fidia vinavyoakisi thamani halisi ya majumba na Ardhi za watu vinatakiwa viangaliwe upya viwe shirikishi na viweze kuakisi thamani halisi ya mali, nyumba na viwanja vya watanzania" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro
"Hivi viwango mnavyovitumia inawezekana vimepitwa na wakati kama ilivyo Sera ambayo imepitwa na wakati na vyote kwa pamoja vinatakiwa vipitiwe, viangaliwe na viundwe upya" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Nawaomba Wizara ya Ardhi, Wananchi wote wanaofidiwa kuanzia Mrusagamba - Rulenge - Tembonikeli - Mlugarama muhakikishe mnatenda haki. Diwani wa Kabanga, Hafidhi Abdallah amenunua kiwanja cha Milioni tano mnataka kumpa laki saba. Haiwezekani! - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Naomba nendeni mkapitie mchakato upya. Government Valuers, Waziri mkatende haki. Mtu anapewa elfu sabini, uliona wapi fidia ya mali ya elfu sabini. Mfanye haraka ili msicheleweshe barabara ya Lami na wananchi wetu waweze kupata haki" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Haiwezekani tunaongelea kupima Vijiji tu, badala ya kutafuta maeneo ya kimkakati, maeneo ya Mpakani, Miji inayokua, maeneo yanayoweza kurudisha fedha haraka, maeneo yenye mzunguko wa fedha ndiyo yakapimwe ili watanzania waweze kumiliki viwanja, waweze kupata hati, waweze kukopesheka na nchi iweze kuendelea" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Ifike mahali makusanyo yanayotokana na Ardhi yaweze kutusaidia watanzania kujiendesha kama Taifa. Eneo hilo halijatendewa haki vizuri. Ninasikitika kuona kinachoendelea" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Shilingi Bilioni 80 zina uwezo wa kupima viwanja 368,000 kwa miaka mitano. Viwanja 300,000, Shilingi Bilioni 51 ikitengwa itarejesha Shilingi Bilioni 80 katika kipindi kilekile. Wastani wa malipo kwa mwananchi ni kati ya elfu 20 mpaka laki mbili kwa kiwanja kimoja" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Upimaji wa Ardhi unalipa. Unatumia Bilioni 51.5 unarudhisha Bilioni 80. Ni kwanini tusitenge fedha tukaenda kupima Ardhi ya watanzania? Ni sababu ipi inaleta kigugumizi kutenga fedha? - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Ofisi za Ardhi zilizopo Ofisi za Serikali za Mitaa hazina fedha kuendesha shughuli za upimaji na matokeo yake hakuna kazi kubwa inayofanyika. Ofisi zimegeuka kutegemea wapimaji binafsi ambao wanakwenda kupima maeneo madogo yasiyotosheleza" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara
"Ninaomba Serikali iwaachie asilimia 30 ya makusanyo yote yanayotokana na Ardhi ili Ofisi ziweze kujiendesha na zifanye upimaji" - Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara