Mbunge Ole Sendeka awasha Moto bungeni kuhusu ripoti ya CAG

Mbunge Ole Sendeka awasha Moto bungeni kuhusu ripoti ya CAG

Ndo mana hatuendelei hii nchi. Sasa wanakula kabisa jasho la wananchi kujadili pongezi kwa kiongozi? Aibu zao mtaani kilio kila kona wao wanapongezana. Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa
 
Anapika data kwa madhumuni gani hasa?!
Kuisaidia serikali, au kuumiza watu?!
Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza fanyia kazi ripoti ya CAG ,thus why huwa inatupwa kwenye dustbin , ni story flan hv ya kuwafanya watanzania wawe busy na kuongea
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza fanyia kazi ripoti ya CAG ,thus why huwa inatupwa kwenye dustbin , ni story flan hv ya kuwafanya watanzania wawe busy na kuongea
Ina maana imejaa uzushi? Ofisi hiyo iwe ya Kwanza kufutwa kabla ya kuyafuta mashirika yasiyo na tija.
 
Ole Sendeka hana jipya. Anatumika kama Toillet paper tuu
 
Serikali huwa haitekelezi/inapuuza mapendekezo ya CAG.
-Serikali inapokea taarifa ya CAG na Takukuru -kuonyesha wapiga kura na dunia kuwa kuna taasisi huru inayoangalia utendaji wa Serikali yao.
-Lakini mapendekezo na ushauri wa taasisi hizi hautekelezwi.
Kwa mfano, Mwaka jana CAG alishauri Serikali iwalipe fidia na riba kwa wananchi wa Kigilagila,Kipawa na kipunguni ambao walihamishwa na Serikali kupisha ujenzi wa uwanja wa ndege terminal 3,
- Lakini mpaka leo hii hakuna dalili za kutekeleza ushauri au pendekezo hilo.
-Watu wa kipunguni ndiyo kwanza wanafanyiwa tadhimini upya na wananchi wa Kigilagila na Kipawa bado kulipwa 6% kwa kila mwaka Kama alivyo agiza CAG .
- Tadhimini ya awali ilikuwa mwaka 1997 na wananchi waliambiwa wasiendeleze makazi yao,hii ina maana majengo yao yamegeuka kuwa magofu,
-Kufanya tadhimini upya 2022/2023 huwezi kupata thamani halisi ya mali zao.
-Maagizo haya,ni kwa maeneo yote ambayo CAG aliagiza Serikali na taasisi zake kulipa fidia kwa wadai, matokeo yake wananchi wanaishi kwenye maisha magumu.

Ushauri
1). Serikali iwe inatekeleza mapendekezo/maagizo ya CAG ili kuondoa mtindo wa hoja kujirudiarudia.
2).Wafadhili/wadaawa wasiwe wanaishia kushuhudia taarifa ya CAG na Takukuru,bali wawe wanafuatilia utekelezi wa hoja za CAG na Takukuru kivitendo.
3).Bunge kufuatilia utekelezaji wa hoja za CAG,ili kupunguza hoja za ukaguzi na ongezeko la riba kwenye madai mengi ya Serikali.
4). Watendaji wa Serikali wajitafakari kwa kuchelewesha utekelezaji wa maagizo ya CAG na madai mengine fedha zilitolewa na Wafadhili au Serikali ilikopa kwa ajili ya miradi hiyo
 
Ktk Azimio Maalum la Kumpongeza Rais Samia kwa uongozi mzuri, kupitia Bunge la 12 mkutano wa 11 kikao cha Kwanza, Ole Sendeka awasha Moto.

Alianza kwa kumsifia Sana Rais Samia lakini mwishoni akaanza kwa kulaumu waliotajwa Ubadharifu Ripoti ya CAG kuenedelea ofisini hadi Sasa.

Kadai wasipojiuzulu na kujisalimisha, Basi kupitia Mkutano huu Bunge lifanye maamuzi dhidi ya wenye viburi na jeuri hao.

Amemtaka Rais achukue hatua vinginevyo yeye kwa kutumia Bunge hili atashawishi wabunge wachukue hatua juu ya watumishi mafisadi.

Wabunge wengine pia wamekuwa na mawazo Kama ya Sendeka na kudai Tanzania hakuna mtu wa kujiuzulu hadi tu aoneshwe mlango wa kutokea. Wamedai wakati wa Bunge kuonesha Meno yake ni Sasa.

Waliounga miongoni mwao ni kitila Mkumbo aliyechangia baada ya Sendeka, Saashisha Mafue, Mwakasaka na wengine wengi.
Mkwara mbuzi tu huu, hawana lolote na hawawezi kuchukua hatua zozote, wizi mkubwa ni chama kinahusika. Kama Pesa za 10% ni za madiwani wao ndio wenye power nazo na hawawezi kufanya lolote sababu ndio chawa wao. Shida kubwa ni Chama ndio waliokuwa wanatetea wakati tunapinga na walikuwa wanasema wanatekelza ilani yao. Presidaa mwenyewe anataka wakae kitako, we uliona wapi mambo haya
 
Wabunge wa mchongo walioingia kwa mchongo, wameanza kujipendekeza
 
Ktk Azimio Maalum la Kumpongeza Rais Samia kwa uongozi mzuri, kupitia Bunge la 12 mkutano wa 11 kikao cha Kwanza, Ole Sendeka awasha Moto.

Alianza kwa kumsifia Sana Rais Samia lakini mwishoni akaanza kwa kulaumu waliotajwa Ubadharifu Ripoti ya CAG kuenedelea ofisini hadi Sasa.

Kadai wasipojiuzulu na kujisalimisha, Basi kupitia Mkutano huu Bunge lifanye maamuzi dhidi ya wenye viburi na jeuri hao.

Amemtaka Rais achukue hatua vinginevyo yeye kwa kutumia Bunge hili atashawishi wabunge wachukue hatua juu ya watumishi mafisadi.

Wabunge wengine pia wamekuwa na mawazo Kama ya Sendeka na kudai Tanzania hakuna mtu wa kujiuzulu hadi tu aoneshwe mlango wa kutokea. Wamedai wakati wa Bunge kuonesha Meno yake ni Sasa.

Waliounga miongoni mwao ni kitila Mkumbo aliyechangia baada ya Sendeka, Saashisha Mafue, Mwakasaka na wengine wengi.
Yeye mwenyewe anataka kudhulumu shamba la marehemu yese,sasa anatofauti gani na hao wapigaji
 
Ifike mahala hili bunge kama vipi lifutwe tujue moja kuwa hatuna bunge.

KATAA UALIMU NI LAANAAAAA
 
Back
Top Bottom