Pre GE2025 Mbunge Ole Sendeka katika bifu kali na RC Sendega agoma kumpigia magoti, magoti yake atayapiga kwa Rais Samia

Pre GE2025 Mbunge Ole Sendeka katika bifu kali na RC Sendega agoma kumpigia magoti, magoti yake atayapiga kwa Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu bogasi, sasa kama yu radhi kupiga magoti kwa rais, kwanini ashindwe kupiga magoti kwa muwakilishi wa rais mkoani. Ama ndio Uchawa kwa raisi kama mtu na sio kwa mamlaka ya uraisi wenyewe.
 
Ndio umuhimu wa Viongozi wa Mkoa kuchaguliwa unaonekana sasa, mpambano wa Kiongozi wa kuchaguliwa na Kiongozi wa kuteuliwa nani zaidi.
 
Siku ya jana Katika kipindi cha bunge jioni Mbunge Mkongwe na aliyewai kuwa Rc, na aliyekuwa mpambe au chawa wa Hayati Edoward Lowassa wakati wa siasa za urais mwaka 2010 Christophe Ole Sendeka amelalamika bungeni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendega amekuwa akiwaweka Lokapu viongozi mbalimbali katika mkoa huu, huku akiongeza kuwa Mkuu wa Mkoa huyu ana mgombea wake wa ubunge amble yeye ana mashaka nae wala hamugopi katika UCHAGUZI wa 2025

Vita ya uchaguzi nani ya CCM imeanza, lakini la pili je kunasababu ya wakuu wa mika na wakuu wa wilaya kuendelea kuwa viongozi Hawa katika ngazi ya uongozi katika nchi

Nimekuwekea clip Yale bendeka hapa chini msikilize anavyolalamikia utawara bora?! utawara bora upi anaohitaji au kwa sababu amebanwa yeye?!

Naona watu wanamshambulia mtoa hoja Ole Sendega badala kusikiliza, kuielewa na kujadili hoja yake...

TUKIRUDI KWENYE HOJA, ni kuwa, mimi naona tatizo kubwa zaidi la viongozi kugeuka miungu watu, untouchable...

Na ni Tanganyika tu kuwa kiongozi wa kuja au kuteuliwa na Rais anaweza kumwamuru kiongozi wa kuchaguliwa na wananchi ampigie magoti...!!!

Iweje kiongozi kama Mkuu wa Mkoa (RC) atumie madaraka yake vibaya (abuse of power) kwa kuonea watu? Hii impunity inatoka wapi?

Polisi nao ni Kwanini wanatii amri haramu ya RC kwa kuwa detain watu wasio na makosa na kinyume cha sheria kwenye selo zao..?
 
Wakubaliane tu either Sendega aondoe "g" aweke "k" au Mzee Sendeka aondoe "k" aweke "g" wawe kitu kimoja
 
Back
Top Bottom