Naomba msaada kwa anayeweza kupenyeza ujumbe huu kwa Mh.Mbunge Saashisha Mafue wa Jimbo la Hai na Serikali sikivu ya Ccm.
Hivi karibuni Serikali ilianza zoezi la kusambaza nguzo za umeme wa Rea kwenye vitongoji kadhaa vya wilaya ya Hai.
Kwenye kitongoji Cha MLIMAFARU kilichopo kijiji Cha Mbatakero zilishushwa nguzo nyingi tu na zikahifadhiwa pembeni ya Barabara ya Longoi-Sadala Kwa Kiria Nguzo hizi mara moja zikaanza kuchimbiwa kwenye baadhi ya kaya huku baadhi ya kaya zikiwa hazijawekewa nguzo.
Wananchi tukaanza kuuliza inakuwaje kaya zingine hazipati nguzo hatukupata majibu sahihi kwa sababu hata Viongozi wa kijiji na Kitongoji hawajui hasa sababu.
WIki moja iliyopita,ikaja gari na kupakia nguzo zilizokuwa zimesalia na kuondoka nazo wakaacha nguzo nne pekee chini.
Kuna kaya ziko pembezoni kabisa ya barabara hazipewa nguzo,na kuna kaya zipo Mita kama 300 nazo hazijapata nguzo.Tunapomhoji msimamizi wa mradk anasema umeme unaenda kwa awamu.Sasa Iweje umruke Mtu halafu uwafungie wengine halafu useme ni kwa awamu?
Kuna familia kama ya kwangu mfano,tuna kaya 10 zipo sehemu moja,ambapo kwa juu umepita umeme wa 3 Phase kwenda kwa Mwekezaji.Nasi hatupati umeme ingali tunazo nguzo za umeme zimekatiza mashambani mwetu.Inawashinda Nini kutufikishia huo umeme kupitia nguzo hizo? Mbona maeneo mengine kwenye wilaya hii mmeifanya hivyo?
Anayesimami mradi tulimuuliza kwanini wengine hatupati umeme akasema kitongoji kimepewa nguzo 40 pekee.Tulipomuuliza kama nguzo walizochimbia zinafika 40 akasema tusimfundishe kazi.Hivi inawezekanaje kwa kitongoji chenye kaya zisizofika 50 ugawe umeme kwa awamu? Ndio agenda ya Serikali?
Jimbo la Hai sehemu ambayo ilikuwa haijafikiwa na umeme tangia nchi ipate uhuru ni ukanda wa tambarare,kwa bahati tumempata mbunge anayeshughulikia maendeleo ya wote,inakuwaje juhudi hizi zinakwamishwa kwa makusudi?
Serikali ilijinasibu kuwa,inafikia vitongoji kwa huduma ya REA mwaka huu,inakuwaje nguzo zinazokuwa zimepangwa kuwafikishia huduma ya umeme wananchi kitongoji chetu zibebwe na kupelekwa wanakojua wao ingali bado kaya zaidi ya 20 hazijapata nguzo? Ndio wanatengeneza madili?
Huku mtaani Mheshimiwa mbunge hawa jamaa wamekula dili na madalali.Wanatuambia ukitaka upewe nguzo wanakupa namba ili uwapigie muelewane.Huo ndio utaratibu wa Serikali?Kuna wakupewa umeme Bure na wa kukaa na kuelewana kwanza?
Serikali inafahamu lolote kuhusu hujuma hii?Mbunge wetu mpendwa unafahamu uozo huu?
Kwa bahati mbaya,baadhi ya madalali wa huo ushenzi ni baadhi Viongozi wa vitongoji na wengine ni wanaojinasibu kuwa makada.Hawa ndio wanakuharibia zaidi Mh.Mbunge na ndio wanaofiisha juhudi za Serikali kuwafikishia huduma ya umeme wananchi kwa usawa.
Kumbe basi tunakuomba Mh.Mbunge na taasisi za Serikali kumulika zoezi la usambazaji umeme kwenye kitongoji chetu.Umegubikwa na ujanja ujanja,upendeleo na unaziacha kaya nyingi zikiwa hazijafikiwa na huduma ya umeme.Hii inaathiri maendeleo yetu na Dhamira ya Serikali katika kutoa huduma Bora za nishati kwa wananchi.
0767 14 16 43